Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli Akimsalimia Muigizajiwa Filamu za Maarufu wa Bongo Movie King Majuto Katika Hospitali ya Tumaini Dar es salaam |
Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth leo wamemtembelea mchekeshaji maarufu nchini, King Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini akipatiwa matibabu ya tezi dume.
Mbali na Mzee Majuto ambaye jina lake halisi ni Amri Athuman, Rais Magufuli amewajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali hiyo kuanzia wodi namba tatu mpaka nane.
Mzee majuto aliyejipatia umaarufu maigizo ya ucheshi amemshukuru Rais Magufuli na kumpongeza kwa kusimamia sekta ya afya kwani ameshuhudia huduma nzuri katika hospitali hiyo tangu alipolazwa.
“Hatua anazochukua Rais Magufuli zimerejesha nidhamu na uchapakazi, tangu nimefika hapa nimehudumiwa vizuri naamini nitapona haraka na kurejea katika ujenzi wa Taifa,” amesema.
Pia amempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kusimamia maslahi ya Taifa na kwamba anamuombea awe na afya njema ili aendelee kuiongoza nchi vizuri.
Aidha, King Majuto amemuombea Rais Magufuli aendelee kutekeleza majukumu yake ya kuongoza nchi vizuri, na amebainisha kuwa hatua zinazochukuliwa na Serikali zimerejesha nidhamu, zimeongeza uchapakazi, zimesaidia kukabiliana na wizi na zimeongeza heshima ya nchi.
Chanzo: Tovuti ya Mwananchi
Chanzo: Tovuti ya Mwananchi