Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani
Iringa ,limepitisha azimio la mpango
mkakati wa kuongeza vyanzo vya mapato
kwa kukitangaza rasmi kivutio kikubwa na cha kipekee hapa duniani ambacho ni
bwawa la maajabu la Mpanga Tazara lililopo kata ya Mpanga Tazara Halmashauri ya
Mufindi ambalo linamaajabu ya kuwa na visiwa vinavyoelea juu ya maji na kuhama
kutoka sehemu moja hadi nyingine vikiwa
na uoto wake wa asili
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe. Festo Mgina,
ameridhia hoja hiyo baada ya kuibuliwa
na mjumbe wa baraza hilo Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Ernei Nyeho, wakati akichangia
hoja katika kikao cha baraza.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa wa kuwa na mipango kabambe juu ya
bwawa letu la Mpanga Tazara, tunatakiwa kutangaza majabu yaliyopo katika bwawa
hili ili kuvutia watalii wengi na hatimaye kupata fedha kwa ajili ya
Halmashauri hivyo kuchochea maendeleo” alisema Nyeho.
Kama ishara ya kukubaliana na Diwani huyo, Mwenyekiti wa
Halmashauri Mhe. Festo Mgina, ameiagiza kamati ya fedha uongozi na mipango
ishughulikie suala hilo na kuliweka katika Mpango mkakati wa Halmashauri pamoja
na kuiagiza kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira kuanzisha mchakato huo kwa
mujibu wa kanuni.
Aidha, Mhe Mgina amesema mkakati
wa kwanza uwe ni kuimarisha
barabara ili kuwe na urahisi wa kufika eneo hilo la maajabu ambalo kwa sasa linafikika kirahisi kwa kutumia usafiri wa
treni.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imepokea Watendaji wa kata 11 kutoka sekretalieti ya ajira katika utumishi wa umma, watendaji hawa wanatarajiwa kutatua chanagamoto ya upungufu wa watumishi wa kada hiyo katika ngazi ya kata baada ya kuondolewa kwa kundi kubwa la Watumishi wakati wa Sakata la kihistoria la vyeti feki.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye pia ni Mwanasheria wa Halmashauri Wakili Agape Fue, akizungumza wakati wa kikao cha Baraza |
Makamu Mwenyeki wa Halmashauri Mhe Ashery Mtono akiongoza sala ya kuliombea Baraza kabla ya kuanza kwa kikao |
Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Nyeho, aliposimama kujenga hoja ya kulitangaza bwawa la Mpanga Tazara na Maajabu yake |
Sehemu ya Watendaji Kata 11 wakitambulishwa mbele ya Baraza |
Sehemu ya Madiwani wakifuatilia kwa makini mijadala wakati wa kikao |