Baada ya Serikali
kuajiri watumishi wapya wa sekta ya Afya mnamo mwezi Julai mwaka huu,
Halmashari ya Wilaya ya Mufindi imepokea jumla ya watumishi hamsini na nne (54)
walitawanywa katika vituo vya Afya na Zahanati za Halmashauri ili kupunguza
changamoto ya upungufu wa wataalamu wa sekta hiyo.
Watumishi ambao
wameripoti na kupangiwa vituo vya kazi ni pamoja na wauguzi ishirini na
mbili (22), Matabibu ishirini na saba (27), wataalamu wa Maabara wawili (02),
wataalamu wa dawa watatu (03), pamoja na Mganga mmoja (01)
Mgawanyo wa watumishi
hawa katika vituo vya Afya na Zahanati umezingatia vigezo mbalimbali kama vile
kupelekwa kwenye vituo vipya, uhitaji wa watumishi katika vituo vinavyotoa au
vinatarajia kutoa huduma ya upasuaji, kupangiwa vituo ambavyo vilikumbwa na
upungufu wa rasilimali watu baada ya zoezi la kuwaondoa watumishi
wenye vyeti feki, kustaafu kwa watumishi sanjari na baadhi yao kwenda
kujiendeleza kitaaluma.
Aidha, baada ya
mgawanyo huo hakuna kituo cha Afya wala Zahanati ya Halmashauri ambayo
imefungwa kwa kukosa wataalamu wa kotoa huduma, lakini pia kwa kuwa na
wataalamu wenye weledi kwenye vituo vyote, kutasadia kukidhi moja kati ya
sharti muhimu la kupata fedha kutoka kwa wahisani zitakazo saidia kuendelea
kuiboresha sekta muhimu ya Afya.
Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi yenye majimbo mawili ya uchaguzi, inajumla ya Zahanati hamsini na
tatu (53) pamoja na vituo vya Afya sita (06). Uongozi wa Halmashauri tunaishukuru
Serikali kwa kutupatia idadi kubwa Watumishi kwa wakati mmoja.