Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limejadili, kuridhia na kupitisha rasimu ya bajeti yenye zaidi ya shilingi bilioni 62.926, ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa Fedha 2018/2019, ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni Bilioni 4.162 kati ya Fedha zote.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwenye kikao maalum cha Baraza, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Isaya Mbeje, amesema, Halmashauri inatarajia kukusanya, kupokea na kutumia zaidi ya Bilioni 62.926, ambapo kati ya Fedha hizo Bilioni 40.728 ni Fedha kutoka Serikali kuu maalum kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, Bilioni 17.205 zimeelekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo huku Bilioni 4.992 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Mbenje ambaye pia ndiye Afisa Mipango wa Halmashauri, amevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2018/2019 kuwa inaangazia ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika kwa miaka ya nyuma hususani ukamilishaji wa Majengo ya sekta ya Afya na Elimu, Ukarabati wa Madarasa chakavu ya baadhi ya Shule za Msingi, ukusanyaji Mapato kwa njia ya kielekroniki, Kutoa huduma bora za kijamii, kuinua uchumi wa wananchi na kuimarisha Miundombinu.
”Mhe Mwenyekiti rasimu hii ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019, rasimu hii itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI Pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango kablaya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge” libainisha Bw. Mbenje.
Azungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambaye pia ndiye Diwani wa kata ya Mninga Mhe. Festo Mgina, amewataka Madiwani kutoa ushirikiano kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapoto ili yasaidie kuharakisha maendeleo kwa kuzingatia kuwa asilimia 60% Mapato ya ndani yanatakiwa kuelekezwa kwenye miradi ya Maendeleo.
“Mkurugenzi wewe pamoja na timu yako tuendelee kuchapa kazi, tunasifa ya Ushirikiano kati ya timu ya Madiwani na Timu yako, tuendeleee kufanya kazi kwa umoja, uadilifu na ushirikiano Kwani sisi kama Viongozi tunatakiwa kuwa chachu ya Maendeleo”.
Rasimu ya bajeti ya 2018 – 2019, aimeandaliwa kwa kuzingatia, Ilani ya Chama cha tawala CCM, Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2018/2019, Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017, Malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halamashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina Akiongoza Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani cha Kupitisha Rasimu Bajeti ya Mwaka 2018/2019 (Picha na Amani Mbwaga) |
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Bwana Isaya Mbenje akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Madiwani wakati wa kujadili na Kupitisha Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2018/2019 (Picha na Amani Mbwaga) |
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa makini Uwasilishaji wa Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (Picha na Amani Mbwaga) |
Diwani wa Kata ya Madabulo Mhe Enrich Nyeho akichangia Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. |
Mganga Mkuu Wilaya ya Mufindi (DMO) Dkt Fredrick Mugalura akijibu baadhi ya Hoja zilizotolewa naWaheshimiwa Madiwani Wakati wa Kujadili Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi 2018/2019. |
Kaimu Afisa Ardhi Maliasili na Mazingira Bwana Shabani Ardha nae akitoa maelezo kwa baraza la madiwani kwa baadhi ya hoja zilizotolewa na waheshimiwa Madiwani. |
Meza kuu ikiendelea kwa makini kuchambua nakupitisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi mwaka2018/2019. (Picha zote na Amani Mbwaga) |