Monday, November 19, 2018

HATUA ZA KISHERIA KUCHUKULIWA KWA WALIOKAIDI UJENZI WA VYOO BORA HALMASHAURI YA MUFINDI



Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ametoa tathimini ya zoezi la kampeni ya ujenzi wa Vyoo bora kwa kaya za Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Kampeni ambayo iliendeshwa  kwa kipindi cha miezi mitano (05) kuanzia mwezi Juni mpaka Oktoba- 2018.

Akitoa taarifa hiyo kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri amesema, Halmashauri inajumla ya kaya 59, 152 kati ya hizo zilizokaguliwa ni 54,133 kati ya hizo kaya zenye vyoo bora ni 33, 562, sawa na 62% huku kaya yenye Vyoo asili na visivyo kubalika ni 19, 109 sawa na 35% wakati kaya ambazo hazina Vyoo kabisa ni 275, sawa na 0.5%

Mhe. William, amezitaja Kata tisa (09) ambazo bado zinaidadi kubwa ya kaya zisizo na Vyoo kabisa sanjari na idadi kubwa ya Vyoo vya asili ambavyo havikubaliki, kuwa ni pamoja na Kata ya Kibengu, Mapanda, Ihalimba, Idunda, Itandula, Mtwango, Sadani, Ihoanzapamoja na Kata Malangali.

Mkuu wa Wilaya amezitaja Kata kumi (10) ambazo kwa asilimia kubwa zimefanya vizuri, kuwa ni pamoja na Kata ya Mpanga Tazara, Kiyowela, Luhunga, Ihanu, Idete, Igowole, Ikongosi, Igombavanu, Makungu pamoja na kata ya Maduma.

Nataka jamii ijue kwamba  suala la kuwa na choo bora halina mbadala ni lazima kila kaya kuwa na choo bora, tokuwa na vyoo bora ni chanzo cha magonjwa ya mlipuko tunapozungumzia choo bora kwa mazingira ya watu wetu ni choo kilichojengwa kwa matofali, kimeezekwa kwa bati na kimesakafiwa ili iwe rahisi kukifanyia usafi”

Aidha, amebainisha kuwa Ofisi yake inaanda ukaguzi mwingine wa kaya kwa kaya ambao utaenda sambamba na kukamata, kutoza faini na kuwafungulia mashitaka kupitia sheria za Mazingira pamoja na Afya za mwaka 2009 wale wote waliokaidi agizo halali ya serikali na ameongeza kuwa pamoja na baadhi ya Kata kufanya vizuri, bado kunakaya ambazo hazina Vyoo bora.

Hiki ni moja kati ya Vyoo bora


Zoezi la kubomoa w Vyoo visivyo na ubora

Zoezi la kubomoa Vyoo visivyo na ubara