Walimu na Wanafunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wameaswa kutokujihusisha na tabia ya
kugushi mitihani ya Taifa kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha matatizo makubwa
katika maisha yao badala yake waweke juhudi katika kufundisha na kusoma kwa
bidii ili ndoto zao za kufaulu mitihani ziweze kutimia kwa njia halali.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mufindi Bw. Netho Ndilito, wakati akihutubia kama mgeni wa heshima kwenye
Maafali ya kidato cha sita (6) ya Shule kongwe ya Sekondari Malangali iliyopo
kata ya Malangali Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Ndilito, amesema tabia ya kufanya udanganyifu katika mitihani
ndiyo chanzo cha kuwa na vijana wasio na uwezo na ambao hawataweza kushindana
katika soko la ajira la jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Nendeni mkapate division one nyingi, lakini nataka kutoa angalizo
hapo kwenye division one na two, tujipange kimkakati tusijekupata division one
kwa kukugushi mitihani ya kitaifa, hiyo ni mwiko na ogopa kama Ukoma kwani tendo hilo
litaharibu sifa njema ya Mhe. DC na Mkurugenzi pia litaichafua Halmashauri
yetu, litaichafua Shule yenu, msisubutu ku-temper na Mitihani”. Alisema Mkurugenzi
Awali Ofisa Elimu idara ya Sekondari wa Halmashauri Mwal.
Mussa Ally, amebainisha kuwa wahitimu wote 179 wapo vizuri kwa taaluma na
nidham huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.
“Nawasihi
mtumie vizuri siku chache zilizobaki kwa kufanya mandalizi ya mwisho “final
touches” ili muweze kupata division one nyingi hivyo kuendelea kulitangaza jina
la Sekondari ya Malangali.” Aliongeza Ofisa huyo mwenye dhamana ya Elimu.
Malangali Shule iliyoanzishwa Aprili 16/1928 ni moja kati ya
Shule kongwe ambayo viongozi wengi wa hapa nchini walisoma huku mwaka huu jumla
ya wanafunzi 179 wanataria kuketi kwa mitihami ya kuhitimu kidato cha sita
kuanzia jumatatu ya tarehe 06
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilito akihutubia |
Wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji hayupo pichani |
zoezi la kutunuku vyeti kwa wahitimu |
Maandamano kuelekea Uwanja wa Maafali
Mara baada ya kuwasili kwa Mgeni wa Heshima akiambatana na Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri |
No comments:
Post a Comment