Thursday, May 24, 2018

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Aridhishwa, Miradi ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho Akiongea na Wananchi wa Kijiji cha  Igombavanu(Hawapo Pichani) mara baada ya Kuzindua Madarasa 02 katika Shule ya Sekondari Igombavanu
Na Amani Mbwaga Mufindi,
Jumla ya Miradi 06 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.199 imezinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi pamoja na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru, ulipokimbizwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, huku wakimbiza Mwenge kitaifa wakiridhishwa  na viwango vya miradi husika na kutanabaisha kuwa vinaendana na thamani ya fedha zilizotumika.

Ukiwa katika Halmashauri  ya Wilaya ya Mufindi  Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa   Sekondari ya Igombavanu, umezindua klabu ya wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Igombavanu,  ujenzi wa zahanati ya Kijiji pamoja na kukagua mradi wa hifadhi ya mazingira katika msitu wa kupandwa wa Halmashauri Kijiji cha Mtili,  umezindua ujenzi wa Barabara ya lami Kitiru- Itulituli yenye urefu wa Kilometa 14.972, na mradi wa kilimo na Mifugo wa Mwananchi  kata ya Igowole.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu. Charles Francis Kabeho, amewahamasisha wananchi kuwekeza katika elimu kwa kugharamia mahitaji muhimu ya Watoto wao, kama mavazi, viatu, Madaftari  sanjari na kuchangia michango wa Chakula cha mchana kwa wanafunzi wa kutwa  chini ya ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge 2018ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”
Aidha, ameendelea Kuhamasisha kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, VVU/UKIMWI, dawa za kulevya na mapambano dhidi ya Malaria.

Maambukizi ya UKIMWI yameendelea kuwa tatizo kubwa katika Mkoa wa Iringa, mkiongozwa na Mkoa wa Njombe wenye asilimia 11.4, wakati ninyi mnashika nafasi ya pili kitaifa kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.3 hivyo, inatupasa tuchukue hatua za kubadili tabia kwani hali hii ikiendelea hivi ni hatari kwa maendeleo ya Taifa’’ alisema Kabeho

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, Kupitia risala ya utii  kwa mkuu wa nchi, amemuhakikishia  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwamba, Wilaya yake, itaendelea kutekeleza  Maagizo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda, usimamizi wa Mbolea ya ruzuku, kuokoa mifumo ya kiikolojia ya bonde la Mto ruaha mkuu pamoja  na suala la Waalimu Kutojihusisha na Michango ya Wazazi Mashuleni .

Mkesha wa Mwenge uliambatana na zoezi la upimaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI  jumla ya watu 435 walijitokeza kujua Afya zao, kati yao wanaume ni 232 na Wanawake ni 203 ambapo katika zoezi hilo ni watu 04 tu ndio waligundulika kuwa na maambukizi ikiwa ni Wanawake 02 na Wanaume 02.

                                             HABARI KATIKA PICHA
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho Akivishwa Skafu na Kijana wa Skauti Mufindi (Picha na Amani Mbwaga)
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Amina Juma Masenza akivishwa skafu na Kijana wa Skauti Wakati wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2018 yaliyofanyika kimkoa Katika Halmashauri ya Wilaya Mufindi (Picha na Amani Mbwaga)



Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William akivishwa Skafu na Vijana wa Skauti Wakati wa Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2018


Kwaya Ikiimba Wakati wa Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018




Kiongozi wa Mbio za Mwenge akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Iringa Mara Baada ya Kumkabidhi Mwenge Ili Uweze Kukimbizwa Mkoani Iringa (Picha na Amani Mbwaga)

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akisalimiana na Waheshimiwa Wabunge na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi (Picha ana Amani Mbwaga)

Wakimbiza Mwenge Kitaifa mara baada ya kupokelewa Mkoani Iringa (Picha naAmani Mbwaga)


 Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Amina Juma Masenza akisoma Ripoti ya Mkoa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  aliyesimama Upande wa Kushoto kwake(Picha na Amani Mbwaga)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe (Picha ana Amani Mbwaga)



Mkuu wa Mkoan Iringa Mhe Amina Juma Masenza akimkabidhi Rasmi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William tayari kwa Kukimbizwa Katika Halmashauri ya Wilaya Mufindi(Picha ana Amani Mbwaga)



Wakati wa Uzinduzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Igombavanu


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Wa Uhuru Ndugu Charles Francis Kabeho akipata Maelezo Kutoka Kwa Afisa Misitu wilaya ndugu Shabani Adhia Wakati akikagua Mradi wa Shamba la Miti ya Mbao la Halmashauri ya Wilaya Mufindi katika Kijiji cha Mtili

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akigawa Vyandarua kwa kina mama wajawazito na wenye watoto wadogo Mara baada ya Kuzindua Zahanati ya Kijiji cha Mtili

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akizindua Barabara ya Lamii yenye Urefu wa Kilometa 14.972 ya Kituli-Itulituli


Familia ya Mzee Mdemo wakipokea Mwenge wa Uhuru mara baaada ya Kukaguliwa kwa Mradi wa Kilimo na Ufugaji nyumbani Kwao Igowole (Picha na Amani Mbwaga)








 Mkuu wa Wilaya Iringa Mhe Kasesela(Kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru Kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David (Picha Zote na Amani Mbwaga)