Tuesday, February 19, 2019

MUFINDI YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 53 2019 - 2020



Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imejadili na kupitisha bajeti ya kiasi cha shilingi bioni 53.853 kwa mwaka wa Fedha wa   2019 – 2020.

Bajeti hiyo imegawanyika katika vipengele vinne ambapo Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya ndani inatarajia kukusanya na kutumia shilingi bilioni 6.175, luzuku ya mishahara kwa watumishi kutoka serikali kuu bilioni 39.277, luzuku kwa matumizi mengine bilioni 2.518 wakati Fedha itakayoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ni zaidi bilioni tisa (09).


Aidha, baadhi ya miradi ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa kwa mwaka ujao wa Fedha ni pamoja na kuanzishwa kwa Kituo cha Utangazaji cha Redio, umarishaji wa sekta ya Afya pamoja na miundombinu ya Elimu.

Akibainisha sababu za kupanda kwa makadirio ya Fedha inayotarajiwa kukusanywa na kutumika  na Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya ndani  kutoka Bilioni 4.162 mwaka 2018 – 2019 mpaka bilioni 6.175 mwaka 2019 – 2020,  Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina, amelimbia Baraza kuwa ongezeko hilo linatokana na Halmashauri kuanza kutoza ushuru wa mbao na nguzo kwa asilimia tano ya gharama ya mazao hayo ya Misitu (05).
“ Sababu nyingine ni zinatokana na kuanza  kutoza ushuru wa kuni zinazotumika Viwandani, kutoza ushuru wa utonvu unaovunwa katika shamba la miti la Sao Hill kwa ajili ya kutengeneza gundi, matumizi ya mfumo wa kielectroniki unaotumika kukusanya mapato sanjari na kuwepo kwa takwimu sahihi ya walipakodi hasa katika sekta za biashara Mifugo na kilimo.”

Bajeti ya 2019 – 2020 imendaliwa kwa kuzingatia mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (05) 2016/17 – 2020/21, Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) ya mwaka 2015, Malengo endelevu ya maendeleo, sheria ya bajeti na kanuni zake, mwongozo wa ushirikiano wa kimaendeleo(DCF) Maekezo ya kisekta sanjari na makubaliano mengine ya kikanda ambayo Serikali imeridhia.


HABARI PICHA
Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina kushoto, akiwaongoza Madiwani hawapo pichani, kuipitia bajeti kifungu kwa kifungu, kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilitho.

Mwenyeki wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina  wa kwanza kushoto, Mkurugenzi Bw. Netho Ndilito katikati na mwanasheria wa Halmashauri Bw. Agape Fue kulia, wakiwa wameinamisha vichwa chini wakati wa sala maalum ya Halmashauri kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza.

Sehemu ya wataalam wa Halmashauri wakifuatilia  mwenendo wa kikao wakati wa baraza la Madiwani 


Sehemu ya Madiwani wakiwa  katika kikao cha baraza