Aliyekuwa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambaye pia ni Mkurugenzi mteule wa Pangani Bw. Isaya Mbenje kulia, akimkabidhi nyaraka mbalimbali Mkurugenzi mpya Bw. Netho Nditilo |
Hatimaye Mkurugenzi
Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Netho Ndilito, amekabidhiwa
rasmi Ofisi na kuanza kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi kutoka kwa aliyekuwa kaimu Mkurugenzi Bw. Isaya Mbenje, ambaye pia ni
Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya
Pangani Mkoani Tanga.
Akizungumza kabla ya
makabidhiano wakati wa kikao cha kujitambulisha na kubainisha dira ya uongozi
wake, ametoa rai kwa watumishi wa kada zote kufanya kazi kwa uadilifu,
kuwajibika ipasavyo katika utendaji kazi na kutanguliza uzalendo wakati wote
wanapowatumikia watu.
“Naomba
sana tuwajibike katika kuutumikia umma, mimi kama kiongozi sitakuwa mvumilivu
kwa watu wazembe, watumishi wenye tabia ya kupokea rushwa, watumishi wasio kaa
ofisini kutoa huduma “wanapatikana kwa tochi” watumishi wa namna hiyo
nikiwabaini kupitia vyombo vyangu sitasita kuchukua hatua na nawahakikishia
tutajua”
Mkurugenzi Ndilito,
ameongeza kuwa, anapenda kuona watu wanafanya kazi kwa uhuru na kuifurahia kazi husika lakini
pia akaahidi kusimamia maslahi ya watumishi kadri ya sitahiki ya Mtumishi kama
moja kati ya njia za kuchochea uwajibikaji wenye tija.
NETHO NDILITO NI NANI?
NETHO NDILITO NI NANI?
Mkurugenzi alizaliwa Mwaka 1982
Kabila lake ni Mgogo
Ni Mume mwenye Mke Mmoja na Watoto wawili (2)
ELIMU
Kwa sasa Mkurugenzi Ndilito ni Mtahiniwa wa Shahada ya tatu (3) yaani shahada ya uzamivu PhD katika chuo kikuu huria cha Tanzania akibobea kwenye ( Development Economics)
Shahada yake ya pili, alitunukiwa katika Chuo Kikuu Cha Arusha (university Of Arusha) mara hii akijikita kwenye (Masters In Business Administration)
Shahada yake ya kwanza, aliipata katika Chuo Kikuu cha Mount Meru University akitunukiwa (Bachelor Of Business With Education)
Aidha pia anataaluma ya Uwalimu Kwa ngazi ya DIPLOMA aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Mount Meru.
UONGOZI Katiaka miaka tofauti na taasisi Zaidi ya kumi (10) tofauti ameshika nafasi za uongozi.
Amekuwa Mkufunzi katika Vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa nyakati tofauti.
Ameandika maandiko mabilimbali Zaidi ya ishirini (20)
kwa wasifu Zaidi Tembelea www.mufindidc.go.tz
Picha ikionesha sehemu ya watumishi wakimsikiliza mkurugenzi |
Mkurugenzi mtendaji mpya Bw. Netho Nditilo, akizungumza na watumishi kwenye Ukumbi wa Halmashauri |
Viongozi wakiwa wameketi katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya watumishi |
Aliyekuwa kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Bw. Isaya Mbenje aliyesimama akisistiza jambo kwa Mkurugenzi mpya |
Mkurugenzi Nditilo, akizungumza na Wakuu wa idara na Vitengo |
Mkurugenzi Nditilo, akipokea ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwa ni moja kati ya mwongozo wa utekelezaji wa majukumu yake |
WASIFU KWA UFUPI