Add caption |
Thursday, November 29, 2018
NAIBU WAZIRI NISHATI AKAGUA CHANZO CHA UMEME MWENGA MUFINDI, AWASHA UMEME WA REA KATA YA IKONGOSI
Na Amani Mbwaga
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewasha umeme katika kijiji cha
Ikongosi kilichopo Kata ya Ikongosi na Kufanya ziara ya kutembelea chanzo cha
Umeme kutoka kwa Mzalishaji binafsi MWENGA HYDRO POWER Chini ya Kampuni tanzu ya
RIFT VALLEY ENERGY iliyopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
“Nimefurahi kufika Mwenga
hapa na nadhani ni mradi wangu wa kwanza kufika katika mradi kama huu wa sekta
binafsi tangu nimeteuliwa kuwa naibu waziri wa Nishati katika uzalishaji huu wa
umeme kwa kutumia maporomoko ya maji, nawapongeza sana Mwenga”. anasema Mhe
Mgalu
Katika suala la uhifadhi
mazingira Mhe. Mgalu, ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mufindi
kuchukua hatua na kuhakikisha vyanzo vya maji ikiwemo chanzo cha mto mwenga
vinatunzwa ipasavyo ili kuwa na umeme wa uhakika na wale wanaofanya shughuli za
kilimo karibu na vyanzo vya maji waondolewe mara moja bila kuwaonea haya.
“Tupo katika vita ya kuhakikisha
miradi inayozalishwa kwa kutumia umeme inafanya kazi kama ilivyokusudiwa,
nashukuru Mungu mwaka huu hatujaona athari katika Mtera na Kidatu” alisema Mhe
Mgalu.
Akitoa wito kwa wakazi wa
maeneo ya chanzo cha umeme wa maji Mwenga, amewataka wananchi kuendelea kutii
maagizo ya serikali za mitaa ya kutunza vyanzo vya maji, aidha amewaomba
viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi magumu katika utekelezaji wa usimamizi wa
kutunza mazingira na hasa kuwasihi wananchi wasilime vinyungu kando na vyanzo
vya maji kwa
Kwa upande wake Meneja Mkuu
wa Mwenga Hydro Power chini ya Kampuni tanzu ya Rift Valley Energy Mhandisi
Joel Gomba amesema wameanza kujena mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo
ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwakani ili kuongeza nguvu
kwenye gridi ya Taifa na inategemewa kuzalishwa Megawati 2.4.
Kizungumzia mchango wa
mradi huo, Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally, amesema
MWENGAHYDRO POWER inazalisha kiasi cha zaidi ya Megawati 3.5 MW na kuvisambazia
umeme jumla ya vijiji 32 na wateja 2,800.
TANESCO
Wilaya ya Mufindi inaundwa na Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya
Wilaya Mufindi yenye Kituo cha kupooza umeme Mgololo (220/33/11) Kv, Wilaya ina
hudumia wateja wapatao 16,436 wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Mufindi wateja
wakubwa 108 wa kati 370 na wadogo 15, 958 aidha Wilaya inauwezo wa 30MW
(Capacity) na matumizi ya juu ni 9.5MW.
Naibu Waziri mwenye nguo rangi nyekundu, akijiandaa kukata utepe kama ishara ya kuzindua huduma ya Umeme katika Kijiji cha Ikongosi juu na chini |
Subscribe to:
Posts (Atom)