Thursday, November 29, 2018

NAIBU WAZIRI NISHATI AKAGUA CHANZO CHA UMEME MWENGA MUFINDI, AWASHA UMEME WA REA KATA YA IKONGOSI


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akikagua miundombinu ya uzalishaji Umeme katika Maporomoko ya Mto Mwenga mradi huu, unaendeshwa ya kampuni binafsi ya MWENGA HYDRO iliyopo Halmashauri ya Mufindi
 Na Amani Mbwaga

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewasha umeme katika kijiji cha Ikongosi kilichopo Kata ya Ikongosi na Kufanya ziara ya kutembelea chanzo cha Umeme kutoka kwa Mzalishaji binafsi MWENGA HYDRO POWER Chini ya Kampuni tanzu ya RIFT VALLEY ENERGY iliyopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.

“Nimefurahi kufika Mwenga hapa na nadhani ni mradi wangu wa kwanza kufika katika mradi kama huu wa sekta binafsi tangu nimeteuliwa kuwa naibu waziri wa Nishati katika uzalishaji huu wa umeme kwa kutumia maporomoko ya maji, nawapongeza sana Mwenga”. anasema Mhe Mgalu

Katika suala la uhifadhi mazingira Mhe. Mgalu, ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mufindi kuchukua hatua na kuhakikisha vyanzo vya maji ikiwemo chanzo cha mto mwenga vinatunzwa ipasavyo ili kuwa na umeme wa uhakika na wale wanaofanya shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji waondolewe mara moja bila kuwaonea haya.

“Tupo katika vita ya kuhakikisha miradi inayozalishwa kwa kutumia umeme inafanya kazi kama ilivyokusudiwa, nashukuru Mungu mwaka huu hatujaona athari katika Mtera na Kidatu” alisema Mhe Mgalu.

Akitoa wito kwa wakazi wa maeneo ya chanzo cha umeme wa maji Mwenga, amewataka wananchi kuendelea kutii maagizo ya serikali za mitaa ya kutunza vyanzo vya maji, aidha amewaomba viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi magumu katika utekelezaji wa usimamizi wa kutunza mazingira na hasa kuwasihi wananchi wasilime vinyungu kando na vyanzo vya maji kwa

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mwenga Hydro Power chini ya Kampuni tanzu ya Rift Valley Energy Mhandisi Joel Gomba amesema wameanza kujena mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwakani ili kuongeza nguvu kwenye gridi ya Taifa na inategemewa kuzalishwa Megawati 2.4.
Kizungumzia mchango wa mradi huo, Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally, amesema MWENGAHYDRO POWER inazalisha kiasi cha zaidi ya Megawati 3.5 MW na kuvisambazia umeme jumla ya vijiji 32 na wateja 2,800.


Naibu Waziri wa kwanza kushoto, akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa Meneja wa shirilka la Umeme Wilayani Mufindi Bw. Omary Ally, aliyeshoosha mkono kab
la ya kuzindua huduma ya Umeme katika Kijji cha Ikongosi juu na chini

TANESCO Wilaya ya Mufindi inaundwa na Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya Wilaya Mufindi yenye Kituo cha kupooza umeme Mgololo (220/33/11) Kv, Wilaya ina hudumia wateja wapatao 16,436 wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Mufindi wateja wakubwa 108 wa kati 370 na wadogo 15, 958 aidha Wilaya inauwezo wa 30MW (Capacity) na matumizi ya juu ni 9.5MW.


Naibu Waziri mwenye nguo rangi nyekundu, akijiandaa kukata utepe kama ishara ya kuzindua huduma ya Umeme katika Kijiji cha Ikongosi juu na chini

No comments:

Post a Comment