Monday, February 4, 2019

BARAZA LA MADIWANI MUFINDI LAWEKA MIKAKATI YA KULITANGAZA BWAWA LA MAAJABU MPANGA TAZARA.

Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina, akifungua kikao cha baraza la Madiwani, kulia ni kaimu Mkurugenzi Bw. Agape Fue na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ashery Mtono

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ,limepitisha azimio la  mpango mkakati wa kuongeza vyanzo vya   mapato kwa kukitangaza rasmi kivutio kikubwa na cha kipekee hapa duniani ambacho ni bwawa la maajabu la Mpanga Tazara lililopo kata ya Mpanga Tazara Halmashauri ya Mufindi ambalo linamaajabu ya kuwa na visiwa vinavyoelea juu ya maji na kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine  vikiwa na uoto wake wa asili

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe. Festo Mgina, ameridhia hoja hiyo baada ya  kuibuliwa na mjumbe wa baraza hilo Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Ernei Nyeho, wakati akichangia hoja katika kikao cha baraza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa wa kuwa na mipango kabambe juu ya bwawa letu la Mpanga Tazara, tunatakiwa kutangaza majabu yaliyopo katika bwawa hili ili kuvutia watalii wengi na hatimaye kupata fedha kwa ajili ya Halmashauri hivyo kuchochea maendeleo” alisema Nyeho.

Kama ishara ya kukubaliana na Diwani huyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina, ameiagiza kamati ya fedha uongozi na mipango ishughulikie suala hilo na kuliweka katika Mpango mkakati wa Halmashauri pamoja na kuiagiza kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira kuanzisha mchakato huo kwa mujibu wa kanuni.

Aidha, Mhe Mgina amesema mkakati  wa kwanza  uwe ni kuimarisha barabara ili kuwe na urahisi wa kufika eneo hilo la maajabu ambalo kwa sasa  linafikika kirahisi kwa kutumia usafiri wa treni.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imepokea Watendaji wa kata 11 kutoka sekretalieti ya ajira katika utumishi wa umma, watendaji hawa wanatarajiwa kutatua chanagamoto ya upungufu wa watumishi wa kada hiyo katika ngazi ya kata baada ya kuondolewa kwa kundi kubwa la Watumishi wakati wa Sakata la kihistoria  la vyeti feki.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri  ambaye pia ni Mwanasheria wa Halmashauri Wakili Agape Fue, akizungumza wakati wa kikao cha Baraza
Makamu Mwenyeki wa Halmashauri  Mhe Ashery Mtono akiongoza sala ya kuliombea Baraza kabla ya kuanza kwa kikao

Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Nyeho, aliposimama kujenga hoja  ya kulitangaza bwawa la Mpanga Tazara na Maajabu yake

Sehemu ya Watendaji Kata 11 wakitambulishwa mbele ya Baraza



Sehemu ya Madiwani wakifuatilia kwa makini mijadala wakati wa kikao










No comments:

Post a Comment