Timu za michezo mbalimbali zinazoundwa
na wataumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa, zimeanza
kujifua tayari kwa kushiriki Bonanza la siku mbili ambapo watumishi wa
Halmashauri zote za Mkoani Iringa sanjali na wale wa Makapuni binafsi
watashindana katika michezo mbalimbali kwa lengo la kuadhimisha siku ya amani
duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 ya mwezi wa 09.
Ofisa habari na Mawasiliano wa
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Ndimmyake Mpokigwa Mwakapiso amesema, bonanza hilo litaanza
tarehe 20 mpaka 21 mwezi huu na kufanyika katika viwanja vya chuo Kikuu cha
Mkwawa ambapo watumishi watashindana katika michezo ipatayo 07 ikijumuisha, Mpira
wa Miguu, Mpira wa pete, Mchezo wa mbio za kwenye magunia kwa wanawake na
wanaume, Mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume.
Michezo mingine ni kufukuza kuku kwa wanawake na wanaume, Mchezo
wa kuchukua chungwa kwa mdomo katika maji kwa wanawake na wanaume na Mchezo wa riadha mita 100 kwa wanawake na wanaume.
Akizungumzia maandalizi ya
ushiriki wa Wilaya ya Mufindi Mwakapiso ametanabaisha kuwa maandalizi ya
kushiriki mashindano hayo yanaendelea vizuri na jumla ya wanamichezo 30 watakao
onesha uwezo kupitia mazoezi hayo watachaguliwa kuiwakilisha Wilaya ya Mufindi
katika michezo itakayoshindaniwa.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete