Friday, February 23, 2018

MADIWANI MUFINDI WAPITISHA BAJETI KWA MWAKA 2018/2019 ASILIMIA 60% IMEELEKEZWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO



Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limejadili, kuridhia na kupitisha rasimu ya bajeti yenye zaidi ya shilingi bilioni 62.926, ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa Fedha 2018/2019, ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni Bilioni 4.162 kati ya Fedha zote.

Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwenye kikao maalum cha Baraza, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Isaya Mbeje, amesema, Halmashauri inatarajia kukusanya, kupokea na kutumia zaidi ya Bilioni 62.926, ambapo kati ya Fedha hizo Bilioni 40.728 ni Fedha kutoka Serikali kuu maalum kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, Bilioni 17.205 zimeelekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo huku Bilioni 4.992 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Mbenje ambaye pia ndiye Afisa Mipango wa Halmashauri, amevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2018/2019 kuwa inaangazia ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika kwa miaka ya nyuma hususani ukamilishaji wa Majengo ya sekta ya Afya na Elimu, Ukarabati wa Madarasa chakavu ya baadhi ya Shule za Msingi, ukusanyaji Mapato kwa njia ya kielekroniki, Kutoa huduma bora za kijamii, kuinua uchumi wa wananchi na kuimarisha Miundombinu.

”Mhe Mwenyekiti rasimu hii ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019, rasimu hii itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI Pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango kablaya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge” libainisha Bw. Mbenje.

Azungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambaye pia ndiye Diwani wa kata ya Mninga Mhe. Festo Mgina, amewataka Madiwani kutoa ushirikiano kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapoto ili yasaidie kuharakisha maendeleo kwa kuzingatia kuwa asilimia 60% Mapato ya ndani yanatakiwa kuelekezwa kwenye miradi ya Maendeleo.

“Mkurugenzi wewe pamoja na timu yako tuendelee kuchapa kazi, tunasifa ya Ushirikiano kati ya timu ya Madiwani na Timu yako, tuendeleee kufanya kazi kwa umoja, uadilifu na ushirikiano Kwani sisi kama Viongozi tunatakiwa kuwa chachu ya Maendeleo”.

Rasimu ya bajeti ya 2018 – 2019, aimeandaliwa kwa kuzingatia, Ilani ya Chama cha tawala CCM, Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2018/2019, Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017, Malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa

                       HABARI KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halamashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina Akiongoza Kikao Maalumu  cha Baraza la Madiwani cha  Kupitisha Rasimu Bajeti ya Mwaka 2018/2019 (Picha na Amani Mbwaga)
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Bwana Isaya Mbenje akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Madiwani wakati wa kujadili na Kupitisha Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2018/2019                                  (Picha na Amani Mbwaga)


Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa makini Uwasilishaji wa Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (Picha na Amani Mbwaga)



Diwani wa Kata ya Madabulo Mhe Enrich Nyeho akichangia Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.







Mganga Mkuu Wilaya ya Mufindi (DMO) Dkt Fredrick Mugalura akijibu baadhi ya Hoja zilizotolewa naWaheshimiwa Madiwani Wakati wa Kujadili Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi 2018/2019.
Kaimu Afisa Ardhi Maliasili na Mazingira Bwana Shabani Ardha nae akitoa maelezo kwa baraza la madiwani kwa baadhi ya hoja zilizotolewa na waheshimiwa Madiwani.
Meza kuu ikiendelea kwa makini kuchambua nakupitisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi mwaka2018/2019.                                                (Picha zote na Amani Mbwaga)

Tuesday, February 6, 2018

Kitita cha Shilingi Milioni 100 chakopeshwa kwa Wanawake na Vijana Mufindi


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William kushoto, akimkabidhi Afisa wa Benki mfano wa hundi kama ishara ya kutoa Mikopo kwa Wanawake na Vijana.
Jumla ya shilingi Milioni 100, zimetolewa kwa sharti la Mkopo kwa vikundi vya Wanawake na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, ikiwa ni utekelezaji wa takwa la sheria inayozitaka mamlaka za Serikali za mitaa  nchini kutenga asilimia 10 ya mapato  ya ndani kwa lengo la kuwakopesha vijana na Wanawake ili wajiajiri kupitia shughuli za kijasirimali hivyo kuboresha maisha yao.
Akisoma taarifa ya Mikopo hiyo, Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Hatibu Bwashehe, ametanabaisha kuwa, kati ya vikundi hivyo, vikundi 22 vya wanawake vimekopeshwa jumla ya shilingi Milioni 62, wakati vikundi 15 vya Vijana vimenufaika na Mkopo huo kwa kupata shilingi Milioni 38.

Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi kwa walengwa, mgeni wa heshima katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, amevitaka vikundi hivyo vielewe kuwa, fedha wanazopokea ni Mkopo hivyo, zitumike kulingana na maandiko waliyowasilisha badala ya kuzitumia kwa malengo tofauti kama vile kuchangia harusi au kununua mavazi ya kifahari na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kutorejesha fedha za Serikali.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Ngina, amepongeza mwenendo mzuri ya urejeshaji Mikopo kwa vikundi vilivyokopeshwa kiasi cha shilingi Milioni 300 kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2016 – 2017 na akaongeza kuwa ili  hali ya urejeshaji izidi kuwa bora zaidi, Watendaji wa kata na Vijiji watahusika kufuatilia marejesho hayo kama ambavyo wanahusishwa  kwenye chakato kusajili vikundi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe, amewahimiza Vijana na Wanawake wa Halmashauri hiyo kuendelea kuwasilisha maombi kwa kuwa Halmashauri yake tayari imetenga fedha nyingine kiasi cha shilingi Milioni 140 ambazo watazikopesha baadaye mwezi ujao mara baada ya kukamilisha uchambuzi wa maandiko ambayo yatakuwa yanalenga kuanzisha viwanda Vidogo.

Aidha, wanufaika wa Mkopo huo ambao ni Wanawake na Vijana, wameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli, kwa kuwathamini na kuwapatia mikopo hiyo huku wakiahidi kuzitumia kwa malengo na kurejesha kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe, akizungumza na Viongozi wa Vikundi vya Wanawake na Vijana wakati wa hafla ya  kukabidhi hundi



 

Thursday, February 1, 2018

TAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017/2018


Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba. Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya.

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.


Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.
Bofya hapa chini kuona matokeo

Chanzo:Muungwana