Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akimkabidhi Kitambulisho Mmoja wa Wazee kwa ajili ya kuwawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika hospitali zote za umma hapa nchini. |
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekabidhi vitambulisho 4,500 vya matibabu kwa wazee vyenye thamani ya Shilingi milioni 10 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali kuu, kuzitaka mamlaka za serikali za mitaa nchini, kutoa vitambulisho hivyo ili kuwawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika hospitali zote za umma hapa nchini.
Hafla fupi ya uzinduzi wa zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo, imefanywa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Mhe. Festo Mgina, katika Kata ya Igombavanu iliyopo jimbo pacha la Mufindi kaskazini.
Zoezi la utoaji wa vitambulisho vya matibabu kwa wazee, litatekelezwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya pili itakayoanza mwaka wa fedha 2018/2019 mapema mwezi wa saba, itahusisha utoaji wa vitambulisho 5705 vyenye thamani ya shilingi milioni 23.
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inakadiriwa kuwa na wazee (10,205)
Katika hatua nyingine, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imezindua zoezi la ugawaji wa Baisikeli za magurudumu matatu mahususi kwa watu wenye ulemavu wa viungo waliopo kwenye Kata 27 za Halmashauri, Baisikeli hizi zilitolewa bure ikiwa ni msaada kutoka Shirika la kimataifa la (Free Wheel Chair Mission) ikiwa ni matokeo ya ushawishi wa Halmashauri kwa Shirika hilo.