Wednesday, June 6, 2018

Waziri Ndalichako : “Maria na Consolata ni Mashujaa wa Taifa


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameongoza waombolezaji  kutoa heshima za mwisho kwa Mapacha walioungana Maria na Consolata mkoani Iringa amabapo alizungumza na waandishi wa habari na kusema mapacha hao  Maria na Consolata  ni  mashujaa wa Taifa  na kwamba wameliacha taifa katika simanzi nzito.

"Mara ya mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.

Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo. 

Kwa hisani ya Mpekuzi Blog.

No comments:

Post a Comment