Na Mwandishi Wetu, Mufindi
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Madiwani ya fedha uongozi na mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina imekagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa robo ya nne 2017/2018.
Kamati imetembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa 02 na ukarabati wa madarasa 04 katika Shule ya Sekondari Igombavanu.
Imetembelea lambo la maji ambalo linatumika na Wananchi katika Shughuli za kilimo cha umwagiliaji ikiwemo kilimo cha matikiti maji na unyweshaji Mifugo katika Kata ya Igombavanu, hii ni kutokana na juhudi za wanufaika wa Mfuko wa TASAF kujenga lambo hilo.
Aidha Kamati ilikagua mradi wa ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari ya Mgalo iliyopo kata ya Sadani ambayo Mpaka sasa imejengwa kwa nguvu za Wananchi na Mbunge wao.
HABARI PICHA
|
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Ikikagua Madarasa yaliyokarabatiwa na Serikali tayari kwa matumizi ya Wanafunzi Katika Shule ya Sekondari Igombavanu |
|
Madarasa 04 ya Shule ya Sekondari Igombavanu yaliyokarabatiwa na Serikali |
|
Madarasa Mapya 02 yaliyojengwa na Serikali katika Shule ya Sekondari Igombavanu
|
|
Ukaguzi wa Choo cha Wanafunzi Kikikiwemo cha Walemavu Shule ya Sekondari Igombavanu |
|
Lambo la Maji Lililopatikana kutokana na Juhudi za TASAF Katika Kusaidia Kaya Masikini amblo linatumika katika Kilimo cha Umwagiliaji na Kunyweshea Mifugo Katika Kata ya Igombavanu |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mwenyesuti akipokea Malezo ya Mradi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Igombavanu Katikakti ni Mratibu wa TASAF na Mwisho ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Mufindi |
|
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igombavanu aliyeinama chini akionesha shamba la Matikiti Maji Yanayolimwa kutokana na Umwagiliaji wa Lambo la Maji |
|
Afisa Mtendaji Kata ya Sadani (Kulia) Bwana Romanus Nyigo akitoa Taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Hosteli ya Shule ya Sekondari Mgalo Mbele ya Kamati ya Fedha na Mipango |
|
Kamati Ikikagua Ujenzi wa Hosteli ya Wasichana Iliyojengwa kwa Nguvu za Wananchi Katika Shule ya Sekondari Mgalo |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akipampu maji katika kisima kinachotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgalo Kulia kwake ni Afisa Elimu Sekondari Bwana John Lupenza |
|
Picha zote na Ofisi ya Habari Mawasiliano na Uhusiano Halmashauri ya Wilaya Mufindi |
No comments:
Post a Comment