Add caption |
Thursday, November 29, 2018
NAIBU WAZIRI NISHATI AKAGUA CHANZO CHA UMEME MWENGA MUFINDI, AWASHA UMEME WA REA KATA YA IKONGOSI
Na Amani Mbwaga
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amewasha umeme katika kijiji cha
Ikongosi kilichopo Kata ya Ikongosi na Kufanya ziara ya kutembelea chanzo cha
Umeme kutoka kwa Mzalishaji binafsi MWENGA HYDRO POWER Chini ya Kampuni tanzu ya
RIFT VALLEY ENERGY iliyopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
“Nimefurahi kufika Mwenga
hapa na nadhani ni mradi wangu wa kwanza kufika katika mradi kama huu wa sekta
binafsi tangu nimeteuliwa kuwa naibu waziri wa Nishati katika uzalishaji huu wa
umeme kwa kutumia maporomoko ya maji, nawapongeza sana Mwenga”. anasema Mhe
Mgalu
Katika suala la uhifadhi
mazingira Mhe. Mgalu, ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mufindi
kuchukua hatua na kuhakikisha vyanzo vya maji ikiwemo chanzo cha mto mwenga
vinatunzwa ipasavyo ili kuwa na umeme wa uhakika na wale wanaofanya shughuli za
kilimo karibu na vyanzo vya maji waondolewe mara moja bila kuwaonea haya.
“Tupo katika vita ya kuhakikisha
miradi inayozalishwa kwa kutumia umeme inafanya kazi kama ilivyokusudiwa,
nashukuru Mungu mwaka huu hatujaona athari katika Mtera na Kidatu” alisema Mhe
Mgalu.
Akitoa wito kwa wakazi wa
maeneo ya chanzo cha umeme wa maji Mwenga, amewataka wananchi kuendelea kutii
maagizo ya serikali za mitaa ya kutunza vyanzo vya maji, aidha amewaomba
viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi magumu katika utekelezaji wa usimamizi wa
kutunza mazingira na hasa kuwasihi wananchi wasilime vinyungu kando na vyanzo
vya maji kwa
Kwa upande wake Meneja Mkuu
wa Mwenga Hydro Power chini ya Kampuni tanzu ya Rift Valley Energy Mhandisi
Joel Gomba amesema wameanza kujena mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo
ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwakani ili kuongeza nguvu
kwenye gridi ya Taifa na inategemewa kuzalishwa Megawati 2.4.
Kizungumzia mchango wa
mradi huo, Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally, amesema
MWENGAHYDRO POWER inazalisha kiasi cha zaidi ya Megawati 3.5 MW na kuvisambazia
umeme jumla ya vijiji 32 na wateja 2,800.
TANESCO
Wilaya ya Mufindi inaundwa na Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya
Wilaya Mufindi yenye Kituo cha kupooza umeme Mgololo (220/33/11) Kv, Wilaya ina
hudumia wateja wapatao 16,436 wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Mufindi wateja
wakubwa 108 wa kati 370 na wadogo 15, 958 aidha Wilaya inauwezo wa 30MW
(Capacity) na matumizi ya juu ni 9.5MW.
Naibu Waziri mwenye nguo rangi nyekundu, akijiandaa kukata utepe kama ishara ya kuzindua huduma ya Umeme katika Kijiji cha Ikongosi juu na chini |
Monday, November 19, 2018
HATUA ZA KISHERIA KUCHUKULIWA KWA WALIOKAIDI UJENZI WA VYOO BORA HALMASHAURI YA MUFINDI
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ametoa tathimini ya zoezi la kampeni ya ujenzi wa Vyoo bora kwa kaya za Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Kampeni ambayo iliendeshwa kwa kipindi cha miezi mitano (05) kuanzia mwezi Juni mpaka Oktoba- 2018.
Akitoa taarifa hiyo kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri amesema, Halmashauri inajumla ya kaya 59, 152 kati ya hizo zilizokaguliwa ni 54,133 kati ya hizo kaya zenye vyoo bora ni 33, 562, sawa na 62% huku kaya yenye Vyoo asili na visivyo kubalika ni 19, 109 sawa na 35% wakati kaya ambazo hazina Vyoo kabisa ni 275, sawa na 0.5%
Mhe. William, amezitaja Kata tisa (09) ambazo bado zinaidadi kubwa ya kaya zisizo na Vyoo kabisa sanjari na idadi kubwa ya Vyoo vya asili ambavyo havikubaliki, kuwa ni pamoja na Kata ya Kibengu, Mapanda, Ihalimba, Idunda, Itandula, Mtwango, Sadani, Ihoanzapamoja na Kata Malangali.
Mkuu wa Wilaya amezitaja Kata kumi (10) ambazo kwa asilimia kubwa zimefanya vizuri, kuwa ni pamoja na Kata ya Mpanga Tazara, Kiyowela, Luhunga, Ihanu, Idete, Igowole, Ikongosi, Igombavanu, Makungu pamoja na kata ya Maduma.
“Nataka jamii ijue kwamba suala la kuwa na choo bora halina mbadala ni lazima kila kaya kuwa na choo bora, tokuwa na vyoo bora ni chanzo cha magonjwa ya mlipuko tunapozungumzia choo bora kwa mazingira ya watu wetu ni choo kilichojengwa kwa matofali, kimeezekwa kwa bati na kimesakafiwa ili iwe rahisi kukifanyia usafi”
Aidha, amebainisha kuwa Ofisi yake inaanda ukaguzi mwingine wa kaya kwa kaya ambao utaenda sambamba na kukamata, kutoza faini na kuwafungulia mashitaka kupitia sheria za Mazingira pamoja na Afya za mwaka 2009 wale wote waliokaidi agizo halali ya serikali na ameongeza kuwa pamoja na baadhi ya Kata kufanya vizuri, bado kunakaya ambazo hazina Vyoo bora.
Hiki ni moja kati ya Vyoo bora |
Zoezi la kubomoa w Vyoo visivyo na ubora |
Zoezi la kubomoa Vyoo visivyo na ubara |
Subscribe to:
Posts (Atom)