Saturday, May 4, 2019

JIEPUSHENI NA TABIA YA KUGUSHI MITIHANI – MKURUGENZI MUFINDI




Walimu na Wanafunzi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Mufindi wameaswa kutokujihusisha na tabia ya kugushi mitihani ya Taifa kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha matatizo makubwa katika maisha yao badala yake waweke juhudi katika kufundisha na kusoma kwa bidii ili ndoto zao za kufaulu mitihani ziweze kutimia kwa njia  halali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Netho Ndilito, wakati akihutubia kama mgeni wa heshima kwenye Maafali ya kidato cha sita (6) ya Shule kongwe ya Sekondari Malangali iliyopo kata ya Malangali Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Ndilito, amesema tabia ya kufanya udanganyifu katika mitihani ndiyo chanzo cha kuwa na vijana wasio na uwezo na ambao hawataweza kushindana katika soko la ajira la jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Nendeni mkapate division one nyingi, lakini nataka kutoa angalizo hapo kwenye division one na two, tujipange kimkakati tusijekupata division one kwa kukugushi mitihani ya kitaifa, hiyo ni mwiko na ogopa kama Ukoma kwani tendo hilo litaharibu sifa njema ya Mhe. DC na Mkurugenzi pia litaichafua Halmashauri yetu, litaichafua Shule yenu, msisubutu ku-temper na Mitihani”. Alisema Mkurugenzi

Awali Ofisa Elimu idara ya Sekondari wa Halmashauri Mwal. Mussa Ally, amebainisha kuwa wahitimu wote 179 wapo vizuri kwa taaluma na nidham huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

 “Nawasihi mtumie vizuri siku chache zilizobaki kwa kufanya mandalizi ya mwisho “final touches” ili muweze kupata division one nyingi hivyo kuendelea kulitangaza jina la Sekondari ya Malangali.” Aliongeza Ofisa huyo mwenye dhamana ya Elimu.

Malangali Shule iliyoanzishwa Aprili 16/1928 ni moja kati ya Shule kongwe ambayo viongozi wengi wa hapa nchini walisoma huku mwaka huu jumla ya wanafunzi 179 wanataria kuketi kwa mitihami ya kuhitimu kidato cha sita kuanzia  jumatatu ya tarehe 06

Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilito akihutubia

Wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji hayupo pichani
zoezi la kutunuku vyeti kwa wahitimu

Maandamano kuelekea Uwanja wa Maafali
Mara baada ya kuwasili kwa Mgeni wa Heshima akiambatana na Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri

Wednesday, May 1, 2019

HABARI PICHA: MAY MOSI KIMKOA WILAYANI KILOLO. MATUKIO KATIKA PICHA


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi, akihutubia, pamoja na mambo mengine Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Irimga kuandaa mpango wa muda mrefu wa kuwakopesha Viwanja watumishi wa umma katika Halmashauri zao.

Sehemu ya watumishi wa umma wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa Wilayani Kilolo







Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi, wa pili toka kushoto, akiwa na  Viongozi mbalimbali jukwaa kuu






Burudani za kufufuka mtu zilipamba maadhimisho haya Wilayani Kilolo

Watumishi na viongozi wakijichanganya wakati wa burudani ya kikundi cha ngoma

Mkuu wa Mkoa akihutubia



Add caption

Watumishi wakifuatilia matukio









Mtumishi hodari toka kitengo cha Sheria Mufindi akipokea zawadi ya 500,000 n na mkono wa pongezi toka kwa Mkuu wa Mkoa


Mtumishi hodari toka idara ya Fedha akipokea zawadi ya 500,000 na mkono wa pongezi toka kwa Mkuu wa Mkoa

Mtumishi hodari toka Idara ya ujenzi akipokea zawadi



Mtumishi toka Idara ya Maliasili akipokea zawadi 


Mtumishi toka Idara ya Mipango akipokea zawadi ya Mtumishi hodari



Mtumishi kutoka kitengo cha ugavi akipokea zawadi







Tuesday, April 16, 2019

SKAUTI MUFINDI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI NA MASOMO.




Vijana wanafunzi wanaojiunga na chama cha Skauti wametakiwa kuzingatia maadili pamoja na kufanya vizuri katika masomo yao ili wawe mfano bora kwa wanafunzi   wengine sanjari na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bw. Netho Ndilitho, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya Vijana wa Skauti 909  kutoka Shule za Msingi na Sekondari za Wilaya ya Mufindi yaliyofanyika katika Kata ya Mbalamaziwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Ndilitho amesema, Skauti sio jeshi la kwenda kufanya vurugu katika jamii, bali ni chama ambacho kimeanzishwa kwa nia ya kuisaidia jamii kwa kutanguliza maslahi ya umma na Taifa mbele.

“Kwa hiyo nendeni makawasaidie wenzenu kwa kuwa mfano bora katika jamii, lakini pia mkawe mfano bora kwenye Madarasa yenu huko, lakini pamoja na kuhudhuria mafunzo haya ya Skauti, mhakikishe mnaweka bidii katika masomo yenu, msome kwa bidii kubwa, kwani Mhe. Rais amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwasomesha ninyi bila malipo” amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Awali akisoma risala ya chama hicho, Kiongozi wa Skauti wa Wilaya ya Mufindi Kamishina Zawadi Mwakihwaja, amesema, chama kimefanikiwa kutoa mafunzo ya stadi za  uokoaji, huduma ya kwanza, Afya, uzalendo, mazoezi ya ukakamavu na uvumilivu .

Ndugu Mgeni rasmi, tunaomba kupatiwa oneo maalum la kufanyia miradi ya Skauti kama vile kupanda bustani. Mifugo na kilimo cha mazao kulingana na majira ya mwaka” aliongeza kamishina Mwakihwaja.

Jumla ya Wanafunzi 909 ambapo kati yao Wavulana ni 452 na Wasichana 457 kutoka shule za Msingi saba (07) na Sekondari thelathini na moja (31) wamehitimu mafunzo ya Skauti yaliyofanyika katika kata ya Mbalamaziwa kwa muda wa siku  nne (04)  

Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Mussa Ally, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji


Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanachama wa Skauti wakila kiapo cha uaminifu mbele ya Kamishina Skauti Wilaya

Mkuu wa Chama cha Skauti Wilaya Mufindi Kamishina Zawadi Mwakihwaja akiwaapisha wanachama wa Skauti

Mgeni wa heshima  Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilitho, akikabidhi vyeti kwa wanachama  909 walioitimu mafunzo



Vijana wa Skauti wakipita kwa ukakamavu mbele ya Mgeni wa heshima



Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ndiye Mgeni wa heshima akivishwa Skafu na mmoja wa kijana wa Skauti

Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilito kushoto, akiwa ameketi na Ofisa Elimu Sekondari kwenye moja ya sehemu maalum iliyojengwa na Skauti kwa ajili ya kupunzika baada ya kazi

Mkurugenzi akikagua sehemu ambayo Skauti huitumia kupika chakula


Mkurugenzi Mtendaji  akitoka kukagua sehemu maalum ambayo Skauti huitumia kuoga







Thursday, April 11, 2019

MAZAO YA MISITU SASA KUSAFIRISHWA SAA 24 - RAIS JPM




Mamia ya wakazi wa Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi walipojitokeza kumlaki Mhe. Rais

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia, amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii kuifuta kanuni ya inayozuia usafirishaji wa mazao ya Misitu nyakati za usiku ili kuongeza kasi ya biashara kwa mazao hayo, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa Taifa.

Mkuu huyo wanchi ametoa kauli hiyo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi, wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mji wa Mafinga walijitokeza kwa wingi kumlaki katika eneo la stendi.

Haya na mimi nakubaliana sasa namwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii kuifuta hiyo “regulation” ili mazao hayo yasafirishwe muda wote na wanaohusika na kudhibiti mazao hayo wajipange kufanya ukaguzi nyakati za usiku na naamini  Waziri atafanya hivyo ndani ya wiki moja hivi” alisema Mhe. Rais’

Aidha, Mhe. Rais amesema Serikali iliweka kanuni hiyo  baada ya kuwepo kwa ajali nyingi nyakati za usiku zilizokuwa zikisababishwa na madareva wa maroli ya kusafirisha bidhaa hiyo huku akitoa rai kwa  Madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani watakaporuhusiwa kusafirisha mazoa hayo nyakati za usiku.

Agizo la kufutwa kwa kanuni hiyo, linaigusa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambayo kwa maiaka mingi imekuwa mzalishaji kiongozi wa mazao ya Misitu hapa chini, hususani Mbao na Nguzo ambazo kila uchwao zimekuwa zikisafirishwa kwa maelfu kwenda Mikoa mabalimbali, Afrika na kwingineko duniani.