Mamia ya wakazi wa Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi walipojitokeza kumlaki Mhe. Rais |
Rais wa jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia, amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii
kuifuta kanuni ya inayozuia usafirishaji wa mazao ya Misitu nyakati za usiku
ili kuongeza kasi ya biashara kwa mazao hayo, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi
kwa Taifa.
Mkuu huyo wanchi ametoa
k auli hiyo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi, wakati akizungumza na mamia ya wakazi
wa Mji wa Mafinga walijitokeza kwa wingi kumlaki katika eneo la stendi.
“Haya na mimi nakubaliana sasa namwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii
kuifuta hiyo “regulation” ili mazao hayo yasafirishwe muda wote na wanaohusika
na kudhibiti mazao hayo wajipange kufanya ukaguzi nyakati za usiku na naamini Waziri atafanya hivyo ndani ya wiki moja hivi”
alisema Mhe. Rais’
Aidha, Mhe. Rais amesema
Serikali iliweka kanuni hiyo baada ya
kuwepo kwa ajali nyingi nyakati za usiku zilizokuwa zikisababishwa na madareva
wa maroli ya kusafirisha bidhaa hiyo huku akitoa rai kwa Madereva kuzingatia sheria za usalama
barabarani watakaporuhusiwa kusafirisha mazoa hayo nyakati za usiku.
Agizo la kufutwa kwa kanuni
hiyo, linaigusa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambayo kwa maiaka mingi
imekuwa mzalishaji kiongozi wa mazao ya Misitu hapa chini, hususani Mbao na
Nguzo ambazo kila uchwao zimekuwa zikisafirishwa kwa maelfu kwenda Mikoa mabalimbali, Afrika na kwingineko duniani.
No comments:
Post a Comment