Thursday, January 24, 2019

MUFINDI YA KUSANYA MILIONI 61 KWA SIKU 15 VITAMBULISHO VYA RAIS JPM


Imeelezwa kuwa jumla ya shilingi Milioni 61,760,000.00 zimekusanywa Wilayani Mufindi kama mapato ya Serikali kupitia zoezi la utoaji vitambulisho vya Wajasiriamali Wilayani humo katika kipindi cha takribani siku 15 tangu kuanza kutolewa kwa vitambulisho hivyo mapema mwezi huu.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akizungumza na hii leo january 24 kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho

Takwimu hizo zimebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, alipotoa tathimini ya awali juu ya mwenendo wa zoezi hilo.


Kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika Wilaya ya Mufindi, amesema tangu kuasisiwa kwa zoezi la kuwatambua na kuwapatia vitambulisho vya ujasiriamali Wajasiriamali wa Wilaya hiyo. mpaka hii leo januari 24 -2019 jumla ya wajasiriamali 2773 wameatambuliwa na kupatiwa vitambulisho maalum vilivyotolewa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kiasi hiki cha fedha cha zaidi ya shilingi Milioni 61 kinatokana na makusanyo kutoka Halmashauri zote mbili ambapo, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekusanya jumla ya shilingi milioni 34,760,000,00 kutoka kwa Wajasiriamali 1738 huku Halmashauri ya Mji Mafinga ikikusanya shilingi Milioni 27,000,000.00 kutoka kwa Wajasiriamali 1035”
Aidha, Mhe. William, ametoa rai kwa Wajasiriamali waliopata vitambulisho waendelee kufanya biashara zao  kwa uhuru pasipo kusumbuliwa na mtu yeyote na kuwahimiza wale ambao bado wanaendelea kufanya biashara pasipokuwa na kitambulisho wahakikishe wanapata vitambulisho na kama kipato chao kinazidi Milioni 04 kwa mwaka ni lazima  wawe na  namba ya mlipa kodi kutoka TRA yaani TIN kwani kutokuwa na kimojawapo kati ya hivyo ni kosa na atakayebainika atazuiliwa kuendelea na biashara husika.

Ndugu zangu bado hatujafika hata asilimia 50 na vitambulisho bado vipo stoo, Wilaya yetu ilipewa vitambulisho 10,000 ambapo 5000 kwa Mji wa Mafinga na 5000 Wilaya ya Mufindi hivyo, naziagiza Halmashauri kwamba itakapofika taraehe 15 mwezi wa pili vitambulisho vyote viwe vimekwisha, narudia tena, itakapofika tarehe 15 -02- 2019 vitambulisho vyote viwe mikononi mwa wajasiriamali.” Alitimisha Mkuu wa Wilaya






No comments:

Post a Comment