Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Ally Hapi amepokea maandamano ya Amani kutoka kwa Wafanyakazi Mkoani humo wakimpongeza Rais Dkt. John Magufuli Kuhusu kurudisha utaratibu wa Kikokoto cha zamani kwa Wafanyakazi wanaostaafu ikiwa ni siku ya Mapinduzi na Kusisitiza kwamba Rais amefanya Mapinduzi hivyo anastahili pongezi.
Akitoa hotuba yake hapo jana Mhe. Hapi amesema alichokifanya Mhe Rais Dkt. John Magufuli ni sehemu ya Mapinduzi kwa watanzania kwa hiyo wafanyakazi hii siku ni siku yetu Mapinduzi haya aliyoyafanya yanawagusa watanzania wote, ningeshangaa kama wanairinga tusingemshukuru Mhe. Rais.
Aidha wafanyakazi hao Wamemshukuru Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kusikia kilio cha wastaafu na watumushi wa umma na kuridhia kikokotoo cha zamani kurudishwa.
Hata hivyo wameomba aendelee kusimamamia mabadiliko 2023 ya kikokotoo kipya ili yalete maslahi mazuri zaidi kwa wafanyakazi na hata ikiwezekana basi kivuke asilimia 50% iliyopo kwa manufaa ya wastaafu hao.
Maandamano hayo yemejumuisha wafanyakazi kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Iringa ikiwemo wilaya ya Mufindi, Iringa na Kilolo huku wakishirikiana na Vyama mbalimbali vya wafanyakazi mkoani humo wakati huo Chama cha waalimu Wilayani Mufindi kikiwa na ujumbe wa "Mtumishi aliyestaafu ni Tunu ya Taifa Kustaafu sio dhambi ni Heshima"
HABARI PICHA
Maandamano ya Amani Yakiendelea |
Mmoja wa Wastaafu akitoa Shuhuda jinsi anavyojisikia mara baada ya uamuzi wa Mhe Rais Kurudisha Kikokotoo |
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri William kitoa salamu za Mufindi |
Wafanyakazi mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Ally Hapi Katika Ofisi yake Mjini Iringa Mara baada ya kupokea maandamano hayo. |
Picha ya pamoja(Picha zote na Amani Mbwaga) |
No comments:
Post a Comment