Tuesday, February 19, 2019

MUFINDI YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 53 2019 - 2020



Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imejadili na kupitisha bajeti ya kiasi cha shilingi bioni 53.853 kwa mwaka wa Fedha wa   2019 – 2020.

Bajeti hiyo imegawanyika katika vipengele vinne ambapo Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya ndani inatarajia kukusanya na kutumia shilingi bilioni 6.175, luzuku ya mishahara kwa watumishi kutoka serikali kuu bilioni 39.277, luzuku kwa matumizi mengine bilioni 2.518 wakati Fedha itakayoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ni zaidi bilioni tisa (09).


Aidha, baadhi ya miradi ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa kwa mwaka ujao wa Fedha ni pamoja na kuanzishwa kwa Kituo cha Utangazaji cha Redio, umarishaji wa sekta ya Afya pamoja na miundombinu ya Elimu.

Akibainisha sababu za kupanda kwa makadirio ya Fedha inayotarajiwa kukusanywa na kutumika  na Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya ndani  kutoka Bilioni 4.162 mwaka 2018 – 2019 mpaka bilioni 6.175 mwaka 2019 – 2020,  Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina, amelimbia Baraza kuwa ongezeko hilo linatokana na Halmashauri kuanza kutoza ushuru wa mbao na nguzo kwa asilimia tano ya gharama ya mazao hayo ya Misitu (05).
“ Sababu nyingine ni zinatokana na kuanza  kutoza ushuru wa kuni zinazotumika Viwandani, kutoza ushuru wa utonvu unaovunwa katika shamba la miti la Sao Hill kwa ajili ya kutengeneza gundi, matumizi ya mfumo wa kielectroniki unaotumika kukusanya mapato sanjari na kuwepo kwa takwimu sahihi ya walipakodi hasa katika sekta za biashara Mifugo na kilimo.”

Bajeti ya 2019 – 2020 imendaliwa kwa kuzingatia mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (05) 2016/17 – 2020/21, Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) ya mwaka 2015, Malengo endelevu ya maendeleo, sheria ya bajeti na kanuni zake, mwongozo wa ushirikiano wa kimaendeleo(DCF) Maekezo ya kisekta sanjari na makubaliano mengine ya kikanda ambayo Serikali imeridhia.


HABARI PICHA
Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina kushoto, akiwaongoza Madiwani hawapo pichani, kuipitia bajeti kifungu kwa kifungu, kushoto  ni Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilitho.

Mwenyeki wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina  wa kwanza kushoto, Mkurugenzi Bw. Netho Ndilito katikati na mwanasheria wa Halmashauri Bw. Agape Fue kulia, wakiwa wameinamisha vichwa chini wakati wa sala maalum ya Halmashauri kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza.

Sehemu ya wataalam wa Halmashauri wakifuatilia  mwenendo wa kikao wakati wa baraza la Madiwani 


Sehemu ya Madiwani wakiwa  katika kikao cha baraza 








Tuesday, February 5, 2019

MKURUGENZI MPYA MUFINDI AKABIDHIWA OFISI, ABAINISHA DIRA YAKE


Aliyekuwa kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Mufindi ambaye pia ni Mkurugenzi mteule wa Pangani   Bw. Isaya Mbenje kulia, akimkabidhi  nyaraka mbalimbali Mkurugenzi mpya  Bw. Netho Nditilo 

Hatimaye Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Netho Ndilito, amekabidhiwa rasmi Ofisi na kuanza kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kutoka kwa aliyekuwa kaimu Mkurugenzi Bw. Isaya Mbenje, ambaye pia ni Mkurugenzi  mteule wa Halmashauri ya Pangani  Mkoani Tanga.

Akizungumza kabla ya makabidhiano wakati wa kikao cha kujitambulisha na kubainisha dira ya uongozi wake, ametoa rai kwa watumishi wa kada zote kufanya kazi kwa uadilifu, kuwajibika ipasavyo katika utendaji kazi na kutanguliza uzalendo wakati wote wanapowatumikia watu.

“Naomba sana tuwajibike katika kuutumikia umma, mimi kama kiongozi sitakuwa mvumilivu kwa watu wazembe, watumishi wenye tabia ya kupokea rushwa, watumishi wasio kaa ofisini kutoa huduma “wanapatikana kwa tochi” watumishi wa namna hiyo nikiwabaini kupitia vyombo vyangu sitasita kuchukua hatua na nawahakikishia tutajua”

Mkurugenzi Ndilito, ameongeza kuwa, anapenda kuona watu wanafanya kazi  kwa uhuru na kuifurahia kazi husika lakini pia akaahidi kusimamia maslahi ya watumishi kadri ya sitahiki ya Mtumishi kama moja kati ya njia za kuchochea uwajibikaji wenye tija.



NETHO NDILITO NI NANI?

WASIFU KWA UFUPI

Mkurugenzi  alizaliwa Mwaka 1982
Kabila lake ni Mgogo
Ni Mume mwenye Mke Mmoja na Watoto wawili (2)

ELIMU

Kwa sasa Mkurugenzi Ndilito ni Mtahiniwa  wa  Shahada ya tatu (3) yaani shahada ya uzamivu PhD katika chuo kikuu huria cha Tanzania akibobea kwenye ( Development Economics)

Shahada yake ya pili, alitunukiwa katika Chuo Kikuu Cha Arusha (university Of Arusha) mara hii akijikita kwenye (Masters In Business Administration)

Shahada yake ya kwanza, aliipata katika Chuo Kikuu cha Mount Meru University akitunukiwa (Bachelor Of  Business With Education)
Aidha pia anataaluma ya Uwalimu Kwa ngazi ya DIPLOMA aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Mount Meru.

UONGOZI Katiaka miaka tofauti na taasisi Zaidi ya kumi (10) tofauti ameshika nafasi  za uongozi.

Amekuwa Mkufunzi katika Vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa nyakati tofauti.

Ameandika maandiko mabilimbali Zaidi ya ishirini (20)
 kwa wasifu Zaidi Tembelea www.mufindidc.go.tz



Picha ikionesha sehemu ya watumishi wakimsikiliza  mkurugenzi

Mkurugenzi mtendaji mpya  Bw. Netho Nditilo, akizungumza na watumishi kwenye Ukumbi wa Halmashauri

Viongozi wakiwa wameketi katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya watumishi

Aliyekuwa kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani  Bw. Isaya Mbenje aliyesimama akisistiza jambo kwa Mkurugenzi mpya

Mkurugenzi Nditilo, akizungumza na  Wakuu wa idara na Vitengo

Mkurugenzi Nditilo, akipokea ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwa ni moja kati ya mwongozo wa utekelezaji wa majukumu yake


WASIFU KWA UFUPI


Mkurugenzi  alizaliwa Mwaka 1982
Kabila lake ni Mgogo
Ni Mume mwenye Mke Mmoja na Watoto wawili (2)

ELIMU
Kwa sasa Mkurugenzi Ndilito ni Mtahiniwa  wa  Shahada ya tatu (3) yaani shahada ya uzamivu PhD katika chuo kikuu huria cha Tanzania akibobea kwenye ( Development Economics)

Shahada yake ya pili, alitunukiwa katika Chuo Kikuu Cha Arusha (university Of Arusha) mara hii akijikita kwenye (Masters In Business Administration)

Shahada yake ya kwanza, aliipata katika Chuo Kikuu cha Mount Meru University akitunukiwa (Bachelor Of  Business With Education)

Aidha pia anataaluma ya Uwalimu Kwa ngazi ya DIPLOMA aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Mount Meru.

UONGOZI Katiaka miaka tofauti na taasisi Zaidi ya kumi (10) tofauti ameshika nafasi  za uongozi.

Amekuwa Mkufunzi katika Vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa nyakati tofauti.
Ameandika maandiko mabilimbali Zaidi ya ishirini (20)
 kwa wasifu Zaidi Tembelea www.mufindidc.go.tz








Monday, February 4, 2019

BARAZA LA MADIWANI MUFINDI LAWEKA MIKAKATI YA KULITANGAZA BWAWA LA MAAJABU MPANGA TAZARA.

Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina, akifungua kikao cha baraza la Madiwani, kulia ni kaimu Mkurugenzi Bw. Agape Fue na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ashery Mtono

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ,limepitisha azimio la  mpango mkakati wa kuongeza vyanzo vya   mapato kwa kukitangaza rasmi kivutio kikubwa na cha kipekee hapa duniani ambacho ni bwawa la maajabu la Mpanga Tazara lililopo kata ya Mpanga Tazara Halmashauri ya Mufindi ambalo linamaajabu ya kuwa na visiwa vinavyoelea juu ya maji na kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine  vikiwa na uoto wake wa asili

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe. Festo Mgina, ameridhia hoja hiyo baada ya  kuibuliwa na mjumbe wa baraza hilo Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Ernei Nyeho, wakati akichangia hoja katika kikao cha baraza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa wa kuwa na mipango kabambe juu ya bwawa letu la Mpanga Tazara, tunatakiwa kutangaza majabu yaliyopo katika bwawa hili ili kuvutia watalii wengi na hatimaye kupata fedha kwa ajili ya Halmashauri hivyo kuchochea maendeleo” alisema Nyeho.

Kama ishara ya kukubaliana na Diwani huyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Festo Mgina, ameiagiza kamati ya fedha uongozi na mipango ishughulikie suala hilo na kuliweka katika Mpango mkakati wa Halmashauri pamoja na kuiagiza kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira kuanzisha mchakato huo kwa mujibu wa kanuni.

Aidha, Mhe Mgina amesema mkakati  wa kwanza  uwe ni kuimarisha barabara ili kuwe na urahisi wa kufika eneo hilo la maajabu ambalo kwa sasa  linafikika kirahisi kwa kutumia usafiri wa treni.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imepokea Watendaji wa kata 11 kutoka sekretalieti ya ajira katika utumishi wa umma, watendaji hawa wanatarajiwa kutatua chanagamoto ya upungufu wa watumishi wa kada hiyo katika ngazi ya kata baada ya kuondolewa kwa kundi kubwa la Watumishi wakati wa Sakata la kihistoria  la vyeti feki.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri  ambaye pia ni Mwanasheria wa Halmashauri Wakili Agape Fue, akizungumza wakati wa kikao cha Baraza
Makamu Mwenyeki wa Halmashauri  Mhe Ashery Mtono akiongoza sala ya kuliombea Baraza kabla ya kuanza kwa kikao

Diwani wa kata ya Mdabulo Mhe. Nyeho, aliposimama kujenga hoja  ya kulitangaza bwawa la Mpanga Tazara na Maajabu yake

Sehemu ya Watendaji Kata 11 wakitambulishwa mbele ya Baraza



Sehemu ya Madiwani wakifuatilia kwa makini mijadala wakati wa kikao










Saturday, February 2, 2019

WAGA KUNUFAIKA, MAMILIONI YA UWINDAJI WA KITALII




Mwenyekiti wa Bodi ya WAGA Mhe. Ashery Mtono akisaini Mkataba pamoja na mwekezaji  Bw. Akram Azizi

Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA inayaoundwa na vijiji vitano vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Halmashauri ya Mbalali na Halmashauri ya Iringa imetiliana saini mkataba wa uwindaji wa kitalii wenye thamani ya dola 30,000 za Kimarekani Zaidi ya shilingi 60,000,000 za Kitanzania na kampuni ya Wembere safaris inayojihusisha na shughuli za uwindaji  wa kitalii  hapa nchini.

Mkataba huo uliosainiwa mwanzoni mwa wiki hii na kushuhudiwa na wakuu wa Wilaya za Mufindi na Mbalali pamoja na wajumbe kutoka vijiji vyote vitano vinavyounda jumuya ya WAGA ambavyo ni Kijiji cha Igomaa na Ihanzutwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Nyamakuyu na Nyakadete kwa Halmshauri ya Mbalali huku Halmashauri ya Iringa ikihusisha Kijiji kimoja cha Mauninga.

Mkataba huo unamruhusu mwekezaji kufanya shughuli za uwindaji wa kitalii katika kitalu cha WAGA kwa kipindi cha miaka mitano (05) lakini pia unamtaka mwekezajia huyo kutoa kiasi cha dola 5,000 za Kimarekani sawa na Fedha za Kitanzania Zaidi ya shilingi milioni 10 zitakazotumika kustawisha maendeleo ya Vijiji hivyo.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba kwa niaba ya Jumuiya, Baraza la udhamini la jumuia ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sadani Mhe. Ashely Mtono, amemtaka mwekezaji huyo kuzingatia makubalino yaliyoainishwa katika mkataba ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kujitokeza hapo badae endapo atakiuka makubaliano hayo.

“Nashukuru kwamba mwekezaji amekubali kilakitu kilichopo katika mkataba na sisi tumejiridhisha, lakini tumesaini leo mkataba, naomba azingatie mkataba ili mwisho wa siku mimi niliyesaini kwa niaba ya Jumuiya usije kuniingiza katika matatizo, nayasema haya kwake kwa kuwa yeye ndiye mtekelezajii na kama ni migogogro sehemu kubwa inaweza kutokea upande wake na sitegemei wala sitarajii kuwa Jumuiya inaweza kuanzisha mgogoro”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya uwindaji ya Wembere Safarie Bw. Akram Aziz, amesema kampuni yake itafanya kazi kwa kuzingatia taratibu za nchi pamoja na kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa kupita mkataba uliosainiwa na kusisitiza kuwa wao kama kampuni hawawezi kuwa kikwazo katika kutekeleza yale yote yaliyokubalika kupitia mkataba huo.

“Kwa upande wetu naahidi tutatekeleza kwa vitendo na hatutegemei wala tatutarajii kuwa na mgogolo wowote kilakitu kilichomo ndani ya mkataba kitatekelezwa kama kilivyo kwani sisi sote ni Watanzania na nia yetu ni kujenga nchi yetu ili ifikie kilele cha mafanikio “

Naye Ofisa wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bi, Rachael Nhambu, amefafanua kuwa, Jumuiya za kuhifadhi Wanyamapori zinaundwa kwa mujibu wa sharia 05 ya kuhifadhi Wanyamapori ya mwaka 2019 kifungu cha 31,32 sanjari na kifungu cha 33 pamoja na kanuni ya kusimamia wanayamapori ya mwaka 2019.

 amefafanua kuwa suala la Jamii kumiliki vitalu vya wanyamapori katika maeneo yanayopakana na Hifadhi za Taifa ni kwa Mujibu wa Sheria ya wanyamapori ya Na. 05 ya mwaka 2009 ambayo inaziruhusu jamii zilizo ridhia na kutoa ardhi ambayo ingeweza kutumika kwa shughuli za kijamii kuwa wamiliki wa vitalu vya kuhifadhi wanyamapori na fedha zitakazotokana na uwekezaji huo hurudi katika Vijiji husika ili zitumike  kwa ajili ya kutekeleza na kuendeleza miradi ambayo ni kwa ajili ya maendeleo ya jamii husika.

Ameongeza kuwa Jumuiya ya WAGA imeundwa na Vijiji 05 vya Igomaa, Ihanzutwa, Nyakadete, Nyamakuyu na Mauninga baada ya Vijiji hivyo kutoa maeneo yao na kuamua kuhifadhi wanyamapori badala ya shughuli nyingine.

Zoezi la kusaini Mkataba


 
Mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi katika picha ya pamoja na wajumbe wa jumuiya ya WAGA