Tuesday, April 16, 2019

SKAUTI MUFINDI WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI NA MASOMO.




Vijana wanafunzi wanaojiunga na chama cha Skauti wametakiwa kuzingatia maadili pamoja na kufanya vizuri katika masomo yao ili wawe mfano bora kwa wanafunzi   wengine sanjari na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bw. Netho Ndilitho, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya Vijana wa Skauti 909  kutoka Shule za Msingi na Sekondari za Wilaya ya Mufindi yaliyofanyika katika Kata ya Mbalamaziwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Ndilitho amesema, Skauti sio jeshi la kwenda kufanya vurugu katika jamii, bali ni chama ambacho kimeanzishwa kwa nia ya kuisaidia jamii kwa kutanguliza maslahi ya umma na Taifa mbele.

“Kwa hiyo nendeni makawasaidie wenzenu kwa kuwa mfano bora katika jamii, lakini pia mkawe mfano bora kwenye Madarasa yenu huko, lakini pamoja na kuhudhuria mafunzo haya ya Skauti, mhakikishe mnaweka bidii katika masomo yenu, msome kwa bidii kubwa, kwani Mhe. Rais amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwasomesha ninyi bila malipo” amesema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Awali akisoma risala ya chama hicho, Kiongozi wa Skauti wa Wilaya ya Mufindi Kamishina Zawadi Mwakihwaja, amesema, chama kimefanikiwa kutoa mafunzo ya stadi za  uokoaji, huduma ya kwanza, Afya, uzalendo, mazoezi ya ukakamavu na uvumilivu .

Ndugu Mgeni rasmi, tunaomba kupatiwa oneo maalum la kufanyia miradi ya Skauti kama vile kupanda bustani. Mifugo na kilimo cha mazao kulingana na majira ya mwaka” aliongeza kamishina Mwakihwaja.

Jumla ya Wanafunzi 909 ambapo kati yao Wavulana ni 452 na Wasichana 457 kutoka shule za Msingi saba (07) na Sekondari thelathini na moja (31) wamehitimu mafunzo ya Skauti yaliyofanyika katika kata ya Mbalamaziwa kwa muda wa siku  nne (04)  

Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Mussa Ally, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji


Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanachama wa Skauti wakila kiapo cha uaminifu mbele ya Kamishina Skauti Wilaya

Mkuu wa Chama cha Skauti Wilaya Mufindi Kamishina Zawadi Mwakihwaja akiwaapisha wanachama wa Skauti

Mgeni wa heshima  Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilitho, akikabidhi vyeti kwa wanachama  909 walioitimu mafunzo



Vijana wa Skauti wakipita kwa ukakamavu mbele ya Mgeni wa heshima



Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ndiye Mgeni wa heshima akivishwa Skafu na mmoja wa kijana wa Skauti

Mkurugenzi Mtendaji Bw. Netho Ndilito kushoto, akiwa ameketi na Ofisa Elimu Sekondari kwenye moja ya sehemu maalum iliyojengwa na Skauti kwa ajili ya kupunzika baada ya kazi

Mkurugenzi akikagua sehemu ambayo Skauti huitumia kupika chakula


Mkurugenzi Mtendaji  akitoka kukagua sehemu maalum ambayo Skauti huitumia kuoga







Thursday, April 11, 2019

MAZAO YA MISITU SASA KUSAFIRISHWA SAA 24 - RAIS JPM




Mamia ya wakazi wa Mji wa Mafinga Wilayani Mufindi walipojitokeza kumlaki Mhe. Rais

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia, amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii kuifuta kanuni ya inayozuia usafirishaji wa mazao ya Misitu nyakati za usiku ili kuongeza kasi ya biashara kwa mazao hayo, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa Taifa.

Mkuu huyo wanchi ametoa kauli hiyo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi, wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mji wa Mafinga walijitokeza kwa wingi kumlaki katika eneo la stendi.

Haya na mimi nakubaliana sasa namwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii kuifuta hiyo “regulation” ili mazao hayo yasafirishwe muda wote na wanaohusika na kudhibiti mazao hayo wajipange kufanya ukaguzi nyakati za usiku na naamini  Waziri atafanya hivyo ndani ya wiki moja hivi” alisema Mhe. Rais’

Aidha, Mhe. Rais amesema Serikali iliweka kanuni hiyo  baada ya kuwepo kwa ajali nyingi nyakati za usiku zilizokuwa zikisababishwa na madareva wa maroli ya kusafirisha bidhaa hiyo huku akitoa rai kwa  Madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani watakaporuhusiwa kusafirisha mazoa hayo nyakati za usiku.

Agizo la kufutwa kwa kanuni hiyo, linaigusa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambayo kwa maiaka mingi imekuwa mzalishaji kiongozi wa mazao ya Misitu hapa chini, hususani Mbao na Nguzo ambazo kila uchwao zimekuwa zikisafirishwa kwa maelfu kwenda Mikoa mabalimbali, Afrika na kwingineko duniani.