Tuesday, August 21, 2018

Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya Mufindi yakagua Miradi ya Maendeleo na Kuridhishwa nayo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akipampu maji katika kisima kinachotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgalo Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi na Diwani Kata ya Sadani Mhe Ashery Mtono

Na Mwandishi Wetu, Mufindi
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Madiwani ya fedha uongozi na mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina imekagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa robo ya nne 2017/2018.

Kamati imetembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa 02 na ukarabati wa madarasa 04 katika Shule ya Sekondari Igombavanu.

Imetembelea lambo la maji ambalo linatumika na Wananchi katika Shughuli za kilimo cha umwagiliaji ikiwemo kilimo cha matikiti maji na unyweshaji Mifugo katika Kata ya Igombavanu, hii ni kutokana na juhudi za wanufaika wa Mfuko wa TASAF kujenga lambo hilo.  

Aidha Kamati ilikagua mradi wa ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika Shule ya  Sekondari ya Mgalo iliyopo kata ya Sadani ambayo Mpaka sasa imejengwa kwa nguvu za Wananchi na Mbunge wao.

HABARI PICHA
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Ikikagua Madarasa yaliyokarabatiwa na Serikali  tayari kwa matumizi ya Wanafunzi Katika Shule ya Sekondari Igombavanu


Madarasa  04 ya Shule ya Sekondari Igombavanu yaliyokarabatiwa na Serikali
Madarasa Mapya 02 yaliyojengwa na Serikali katika Shule ya Sekondari
Igombavanu


Ukaguzi wa Choo cha Wanafunzi Kikikiwemo cha Walemavu Shule ya Sekondari Igombavanu
Lambo la Maji Lililopatikana kutokana na Juhudi za TASAF Katika Kusaidia Kaya Masikini amblo linatumika katika Kilimo cha Umwagiliaji na Kunyweshea Mifugo Katika Kata ya Igombavanu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mwenyesuti akipokea Malezo ya Mradi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Igombavanu Katikakti ni Mratibu wa TASAF na Mwisho ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Mufindi

 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igombavanu aliyeinama chini akionesha shamba la Matikiti Maji Yanayolimwa  kutokana na Umwagiliaji wa Lambo la Maji


Afisa Mtendaji Kata ya Sadani (Kulia) Bwana Romanus Nyigo akitoa Taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Hosteli ya Shule ya Sekondari Mgalo Mbele ya Kamati ya Fedha na Mipango
Kamati Ikikagua Ujenzi wa Hosteli ya Wasichana Iliyojengwa kwa Nguvu za Wananchi Katika Shule ya Sekondari Mgalo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akipampu maji katika kisima kinachotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgalo Kulia kwake ni Afisa Elimu Sekondari Bwana John Lupenza


Picha zote na Ofisi ya Habari Mawasiliano na Uhusiano Halmashauri ya Wilaya Mufindi

Monday, August 20, 2018

PROF. SHEMDOE AKABIDHI MIKOBA YA UKURUGENZI HALMASHAURI YA MUFINDI.

 Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe Kulia , ambae kwa sasa ndiye Katibu Talawa wa Mkoa wa Ruvuma  Akimkabidhi Ofisi  na Vifaa Kaimu Mkurugenzi Bwana Issaya Mbeje, Nyuma ni Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akishuhudia Makabidhiano hayo 


Na Mwandishi Wetu Mufindi.
Hatimaye aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe, ambae kwa sasa ndiye Katibu Talawa wa Mkoa wa Ruvuma kufuatia uteuzi wa mkuu wa nchi, amekabidhi rasmi Ofisi na madaraka ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi kwa kaimu Mkurugenzi Ndugu. Isaya Mbenje, kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uongozi katika taasisi za umma.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika ofisini kwa Mkurugenzi mtendaji, Prof. Shemdoe, amewashukuru wakuu wa idara, vitengo na watumishi wote kwa ujumla ambao  walimsaidia kazi kwa juhudi maarifa na uaminifu jambo ambalo limesababisha aonekane na mamlaka za juu na hata kupata madaraka makubwa zaidi.
“Ninyi wakuu wa idara ndio mlioanifundisha kazi huku Serikali za mitaa, wakati nakuja huku nilikuwa sijui kitu, huku tofauti sana na  kule chuo kikuu nilikotoka, kule niljiua leo ninakipindi saa nne, nikitoka darasani najifungia kundika maandiko, ni kweli kwamba Mufindi ndiyo sehemu pekee ambayo kwa kiasi kikubwa nimejifunza uongozi hivyo, popote nitakapokuwa sitaisahau katika maisha yangu”
Aidha, Prof. Shemdoe, amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kutolinganisha uongozi wake na ule wa kaimu aliyemwanchia Ofisi wala kiongozi atakayeteuliwa rasmi kurithi nafasi yake na kusisitiza kuwa binadamu wanatofautiana na hata siku moja hawawezi kufanana kwa kila kitu kwani kila mmoja anamtazamo wake na namna yake ya kuongoza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye ndiye alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo, amempongeza  kwa uadilifu na utendaji mzuri wa kazi na akabainisha kuwa mara zote alitumia taaluma yake kama Profesa kutatua changamoto zilizokuwa zikijitokeza.
Hakika kulikuwa hakuna changamoto ambayo ilikuwa haipati utatuzi kwa Prof, alinisaidia sana kupata suluhisho la mambo mengi hata kwa mambo yangu binafsi, alikuwa kiunganishi sahihi kati ya ofisi ya DC na Halmashauri ni katika kipindi chake uhusiano wa Ofisi hizi mbili ulikiwa imara zaidi, ungeweza kudhani Ofisi ya DC na Mkurugenzi ni moja.”Alisema  Mkuu wa Wilaya.
WASIFU. Prof. Riziki Shmdoe alizaliwa  Wilayani Lushoto Mkoani Tanga Mwaka 1974, alipata Shahada ya tatu ya  uzamivu PHD chuo kikuu cha Ghent kilichopo barani Ulaya Nchini Ubeligiji na kubobea kwenye taaluma ya (Applied Biological Sciences). Mwaka 2001 mpaka 2003 alisoma na kuhitimu shahada ya umahiri (Masters) katika chuo kuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro akijikita kwenye (Management of Natural Resources For Sustainable Agriculture). Mwaka 1997 -2000 alisoma na kuhitimu Shahada ya kwanza ya taaluma ya Misitu katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine  (SUA) Morogoro’
Aidha, 1994 – 1996 kidato cha 5 -6 Shule ya Sekondari SAME
1990 -1993: Kidato cha nne LWANDAME Sekondari
1983 – 1989: NGWERO Shule ya Msingi .

HABARI PICHA
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe akiongea na Watumishi waliokuwa wakikshuhudia Makabidhiano ya Ofisi

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina nae akisaini nyaraka za Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi Mufindi












Picha ya Pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo Mbalimbali vya Halmshauri ya Wilaya Mufindi (Katikati) ni Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William Kushoto kwake ni RAS wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji na Anaye fuatia ni Kaimu Mkurugenzi Bwana Isaya Mbenje, Kulia kwa DC ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina na anaefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya (W) Mufindi Mhe Ashery Mtono (Picha zote na Ofisi ya Habari Mawasiliano na Uhusiano)

Wednesday, August 15, 2018

Mkuu wa Mkoa Iringa Ametoa Siku 90 Wazee Wote Wakabidhiwe Vitambulisho vya Matibabu.


Mkuu Mpya wa Mkoa wa Iringa Mh Ally Salum Hapi akiongea na Watumishi wa Wilaya ya Mufindi wakati wa ziara yake ya kujitambulisha Mapema wiki hii (Picha na Ofisi ya Habari Mawasiliano na Uhusiano Halmashauri ya Wilaya Mufindi)
Mkuu mpya wa Mkoa Iringa Mhe. Ally Hapi, ametoa Siku 90 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa, Kuhakikisha wazee wote Mkoani humo wanatambuliwa na   kupewa vitambulisho vya matibabu bure ili waweze kutibiwa kwenye hospitali yoyote ya umma bila usumbufu.
Mhe. Hapi, ameyasema hayo  wakati akizungumza na watumishi wa umma Wilayani Mufindi katika ziara yake ya kwanza yenye lengo la kujitambulisha kwa watumishi wa umma  Wilayani humo.
“Na Kwenye hili nimesema wazee wasiwafuate Halmashauri kwenda kupewa hivyo vitambulisho bali Halmashauri Kupitia DMO na timu yake mtoke muwafuate wananchi kata kwa kata muwaandikishe, Muwasajili na kisha muwapelekee vitambulisho mahali walipo na baada ya siku 90 nataka nipate mrejesho chanya kuhusu agizo hili”.
Akizungumzia suala  la utendaji kazi, Mhe. Hapi, amewataka watumishi kutofanya kazi kwa mazoea bali kutimiza wajibu wao kwa ubunifu na uaminifu kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria ili kuleta matokeo chanya kwa umma wanaoutumikia.
“Awamu ya tano inazungumzia hapa kazi tu, kwanza ni lazima mkiheshimu chama cha mapindizi maana serikali hii haikujileta yenyewe, pili, lazima watendaji mtoke ofsini na kwenda kuwahudumia wananchi ili kutatua shida zao, kutenda haki na kuwa waadilifu lakini pia  ni lazima tuongeze juhudi za kukusanya mapato ya serikali kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili Halmashauri  zote za Mkoa wa Iringa zisishuke asilimia 90%”alisema Mhe Hapi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Hapi amesema anatarajia kuanza kufanya mikutano ambapo kwa muda wa siku 18 atazunguka kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa na kufanya mikutano isiyopungua mitatu  kwenye kila Tarafa katika mikutano hiyo, atazungumza na wananchi sanjari na kusikiliza kero zao zoezi ambalo litaitwa Iringa Mpya.
Akisoma taarifa ya Wilaya, Mkuu wa wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William, amesema, anaishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa kuendelea kuleta fedha katika Wilaya yake.
Ameongeza kuwa, mwaka 2017/2018 Wilaya ya Mufindi ilipokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha Tsh Bilioni 06 na Milioni 200 kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida.
Tarehe 28 Julai Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Mhe. Ally  Hapi, Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa akirithi nafasi ya Mhe. Amina  Masenza, aliyestaafu kwa mujibu wa sheria, awali Mhe.  Hapi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es alaam.

                         HABARI KATIKA PICHA


Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Salum Hapi  akipokelewa na  Mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William alipowasili Wialayani hapo kwa ajiliZiara yake ya Kwanza ya Kujitambulisha

Mkuu wa Mkoa Iringa Mh Ally Salum Hapi akiongea na Watumishi wa Wilaya ya Mufindi (Picha na Ofisi ya Habari Mwasiliano na Uhusiano Halmashauri ya Mufindi) .
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi na Mji Mafinga wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa Iringa Ally Hapi (Hayupo Pichani) 
Mkuu wa Mkoa Iringa akiongea na Watumishi wa Halmashauri ya WilayaMufindi

Kaimu Chifu wa Wahehe akiongea na watumishi wa Wilaya ya Mufindi ikiwa ni Moja ya Ukaribisho wa RC Mpya Mufindi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akitoa salamu za Shukrani kwa ujio wa Mkuu wa Mkoa 
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi Katikati akiwa katika Picha Ya Pamoja na Machifu wa Iringa Kulia Kwake ni Mkuu wa Wilaya Mufindi na Kushoto kwake ni Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Iringa Rose Tweve na Nyuma Kushoto ni RPC -Iringa Kamanda Juma Bwire
RC-Iringa waliokaa  (katikati) akiwa katika Picha Ya Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mufindi
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Hapi akiongea na Wafanyabiashara wa Stendi ya Mji wa Mafinga alipita kuwasalimia mara baada ya kumaliza ziara yake ya Kujitambulisha Wilayani Mufindi (Picha Zote na Ofisi ya Habari Mawasiliano na Uhisiano Mufindi)