Imeelezwa kuwa jumla ya shilingi Milioni 61,760,000.00 zimekusanywa Wilayani Mufindi kama mapato ya Serikali kupitia zoezi la utoaji vitambulisho vya Wajasiriamali Wilayani humo katika kipindi cha takribani siku 15 tangu kuanza kutolewa kwa vitambulisho hivyo mapema mwezi huu.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akizungumza na hii leo january 24 kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho |
Takwimu hizo
zimebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, alipotoa
tathimini ya awali juu ya mwenendo wa zoezi hilo.
Kiongozi huyo wa ngazi
ya juu katika Wilaya ya Mufindi, amesema tangu kuasisiwa kwa zoezi la
kuwatambua na kuwapatia vitambulisho vya ujasiriamali Wajasiriamali wa Wilaya
hiyo. mpaka hii leo januari 24 -2019 jumla ya wajasiriamali 2773 wameatambuliwa
na kupatiwa vitambulisho maalum vilivyotolewa na Mhe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
“Kiasi hiki cha fedha cha zaidi ya
shilingi Milioni 61 kinatokana na makusanyo kutoka Halmashauri zote mbili
ambapo, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekusanya jumla ya shilingi milioni
34,760,000,00 kutoka kwa Wajasiriamali 1738 huku Halmashauri ya Mji Mafinga
ikikusanya shilingi Milioni 27,000,000.00 kutoka kwa Wajasiriamali 1035”
Aidha, Mhe. William,
ametoa rai kwa Wajasiriamali waliopata vitambulisho waendelee kufanya biashara
zao kwa uhuru pasipo kusumbuliwa na mtu
yeyote na kuwahimiza wale ambao bado wanaendelea kufanya biashara pasipokuwa na
kitambulisho wahakikishe wanapata vitambulisho na kama kipato chao kinazidi Milioni
04 kwa mwaka ni lazima wawe na namba ya mlipa kodi kutoka TRA yaani TIN kwani
kutokuwa na kimojawapo kati ya hivyo ni kosa na atakayebainika atazuiliwa kuendelea
na biashara husika.
“Ndugu zangu bado hatujafika hata asilimia
50 na vitambulisho bado vipo stoo, Wilaya yetu ilipewa vitambulisho 10,000
ambapo 5000 kwa Mji wa Mafinga na 5000 Wilaya ya Mufindi hivyo, naziagiza Halmashauri
kwamba itakapofika taraehe 15 mwezi wa pili vitambulisho vyote viwe vimekwisha,
narudia tena, itakapofika tarehe 15 -02- 2019 vitambulisho vyote viwe mikononi
mwa wajasiriamali.” Alitimisha Mkuu wa Wilaya